NDANI YA MSANII WA WIKI HII....
Sixbert Mubiligi |
Rejoice Blog: Tuanze
kwa kujua majina yako kamili na ikiwa unatumia jina tofauti kwenye kazi zako za
muziki?
Sixbert: Majina
yangu ni Sixbert Eldard Mubiligi, kwenye huduma natumia zaidi Sixbert Mubiligi.
Rejoice Blog: Je,
umeokoka? Unaabudu katika kanisa gani?
Sixbert: Mimi
nimeokoka kweli kweli; ninaabudu kanisa la TAG - nikiwa Morogoro kwangu
ninaabudu TAG Bethel Mwembesongo linaloongozwa na Askofu Mkuu Barnabas Mtokambali.
Nikiwa Mtwara naabudu kanisa la TAG Shangani Miracle Temple chini ya Askofu
George Musa.
Sixbert Mubiligi katika moja ya Mikutano ya Injili |
Rejoice Blog:
Historia yako kwa kifupi ya kuimba, ulianzaje na wapi ulianzia?
Sixbert: Nimeanza
tangu nikiwa mdogo Sunday School Basanza Uvinza Kigoma, na nilipofika umri
wa kutosha kuimba na watu wazima niliimba kwaya ya kwanza ya Neema iliyopo Basanza
Uvinza, ni kwaya ya kanisa la Anglican. Baadaye nikaja Urambo Tabora na
nikaimba kwaya ya ESSACU pale wilayani Urambo. Nilipokuja kwa baba yangu Morogoro
nimeimba kwaya ya Safina pale Anglican Magereza Kihonda. Baadae nilipoanza
kidato cha kwanza ndipo nilipokutana na wapendwa tukatengeneza bendi iliyoitwa
SGS hapo ndipo ulikuwa mwanzo wa kuingia studio hapo ilikuwa 2005 nikiwa kidato
cha tatu na tulifanya kazi kama Maisha bora
Rejoice Blog: Safi
sana. Una historia ndefu kwa kweli katika muziki wa Injili. Katika kuimba
kwako, je, umeshatoa album yoyote?
Sixbert: Yesu
umenipa Heshima na mwaka 2009 nikiwa kidato cha Sita nilifanikiwa
kurekodi albamu yangu iliyoitwa BWANA ATASIMAMA.
Na sasa ninaandaa albamu mpya iitwayo YESU HASHINDWI na albamu ya pamoja kati yangu na rafiki yangu ambae tumeanza nae huduma hii tangu tukiwa sekondari, anaitwa ALFRED MWAKASASA.
Na sasa ninaandaa albamu mpya iitwayo YESU HASHINDWI na albamu ya pamoja kati yangu na rafiki yangu ambae tumeanza nae huduma hii tangu tukiwa sekondari, anaitwa ALFRED MWAKASASA.
Sixbert akiwa na mwimbaji Joshua Silomba |
Rejoice Blog:
Nani anasambaza na kusimamia kazi zako?
Sixbert: Kazi
zangu nasambaza mwenyewe sijapeleka kwa wasambazaji, lakini hizi kazi mbili
itabidi nitafute msambazaji. Kwa upande wa usimamizi bado natafuta mtu
atakayesimamia au hata kampuni ambayo nitafanya nayo kazi.
Rejoice Blog:
Ni msanii gani wa muziki wa Injili anayekuvutia na unapenda kufuatilia kazi
zake?
Sixbert: Mwimbaji
ninavutiwa naya ni Ambwene Mwasongwe na huwa nasikia tu kumfuatilia kazi zake.
Kwa kifupi ndiye Fanuel Sedekia wa wakati huu maana anayatunza mafuta ya
madhabahu katika uimbaji
Rejoice Blog:
Kuna mafanikio gani umeyapata katika kuimba nyimbo za Injili?
Sixbert: Mafanikio
ni mengi cha kwanza uimbaji umenipa digrii Udom na mengine mengi maana
kumtumikia Mungu kuna faida, lakini kubwa zaidi nimepata watu wengi sana ambao
ni wa familia ya Yesu Kristo
Sixbert akiwa na waimbaji wengine studio |
Rejoice Blog:
Umekutana na changamoto gani katika huduma yako ya uimbaji?
Sixbert: Waoh!
Changamoto kubwa ni fedha ambapo huduma hii inahitaji pesa kuliko vile watu
wanavyofikiria. Changamoto nyingine ni baadhi ya watumishi utakuta anakuita
kwenye huduma wewe binafsi alikuambia mtumishi hali ni ngumu lakini ukifika
kwenye mkutano au semina unakutana na muimbaji kutoka Dar ambae anaondoka na bahasha
ya laki saba wewe hata mafuta ya gari hupati. Hii kwangu huwa inaumiza hata
ungekuwa wewe mwandishi ungeumia
Rejoice Blog:
Unaonaje muziki wa Injili hapa Tanzania? Na hasa wa aina unayoimba wewe?
Sixbert: Muziki
wa tanzania unakuwa kila siku, na tasnia inang'aa kwa kweli
Rejoice Blog:
Unatoa ujumbe gani kwa waimbaji wa nyimbo za Injili ambao kwa njia moja ama
nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia hii?
Sixbert: Kama
umeamua kumtumikia Mungu unatakiwa uwa halisi hapo Mungu atayaachilia mafuta
yake juu yako.
Rejoice Blog:
Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unakifanya?
Sixbert: Mbali
na huduma, mimi ni mwalimu wa sekondari Manispaa ya Mtwara pia mjasiriamali
Sixbert akiwa na mkewe Joyce |
Rejoice Blog:
Je, umeoa na una watoto?
Sixbert: Yeah
mimi ni mume wa mke mzuri Joyce Sixbert. Pia Bwana Yesu katuzawadia Mtoto wa kike
anayeitwa Prettyn.
Rejoice Blog:
Una ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa Tanzania?
Sixbert: Niwaombe
watumishi ambao Bwana kawapa kibali cha kuonekana mbele za jamii jitahidini
kutamani kuwawezesha wengine ili familia ya wana wa Asafu ikue maana
binafsi napenda waimbaji waongezeke kila siku. Na pia tuache ukabila kwenye
huduma.
Rejoice Blog:
Na kwa jamii inayoguswa na kuburudishwa na nyimbo za Injili una ujumbe gani
kwao?
Sixbert: Ujumbe
wangu kwa jamii watusapoti, huduma hii inawahitaji wao ili isonge mbele. Amen
Rejoice Blog:
Ahsante sana Sixbert kwa muda wako, Mungu akubariki na kukuinua unavyoendelea
kumtumikia kwa uaminifu
Sixbert: Amen,
ahsante
Huyo ndiye Sixbert Mubiligi,
kijana aliyeanza kumtumikia Mungukwa muda mrefu kupitia uimbaji. Naamini
umepata kumfahamu zaidi kwa angalau hatua moja mbele
Kwa mawasiliano na Sixbert
kwa habari ya huduma unaweza kumpata kupitia namba 0716552795 au barua pepe mubiligis@yahoo.com
~~~ UBARIKIWE ~~~
No comments:
Post a Comment