Watarajiwa hao in courtesy of stockpics |
Watu
wengi inapofika katika swala la kutafuta mwenzi wa maisha,nikiwa na maana mume
au mke huwa inakuwa ngumu sana. Maana wanakuwa hawajui wafanye nini ili waweze
kupata ubavu ambao ndio Mungu amekusudia na sio kuchukua ubavu wa wenzao. Ni
jambo la maana sana unapotafuta au kujiandaa kuwa na mwenzi wa maisha kujua
mambo muhimu yatakayo kusaidia kuepusha kukutana na mwenzi sahihi kutoka kwa
Mungu.
Leo
nitaelezea mambo muhimu matatu tu japo hii itakuwa series ambapo tutaendelea
kueleza zaidi na zaidi juu ya vitu muhimu tunavyoendelea huko mbele.
Mambo
hayo ni;
1.
Maombi
Maombi
ni muhimu sana na yanakufanya uwe na ushirika na Mungu,na unapoomba ni ishara
ya kumwambia Mungu kwamba bila wewe Mungu wangu siwezi. Kuna mchungaji mmoja
alitufundisha ni muhimu kufanya maombi pale ambapo huna picha yoyote
kichwani,maana tatizo la watu wengi ni kwamba wanakwenda kuomba Mungu huku ana
picha ya mtu Fulani,au mwingine anamwambia Mungu ooh Mungu nipe huyu,nataka
kukumbia rafiki hiyo sio njia nzuri.
Wewe
muombe Mungu akupe mwenzi,halafu kama neno lake linavyosema kwamba tukiomba
tuamini kwamba ametupatia na kwamba Mungu si dhalimu maana yeye ni baba atatupa
kitu chema,basi tuamini hivyo.Ukishaomba na kuamini kwamba umepata hata kama
katika hali halisi huoni anza kumshukuru Mungu kwa mwenzi mzuri kutoka kwake.
Mtumishi
mwingine alifundisha unaweza kusema huyo mtu awe na haiba gani n.k,lakini ujue
kwamba Mungu yuko juu ya vyote atakaye kupa ndio sahihi kuliko akili yako
inavyohitaji au kudhani.
Maombi
ni eneo muhimu sana ni vizuri ukawa na mtu ambaye mnaelewana na kiimani mko
katika level moja au yeye amekuzidi mkawa mnaliombea hilo pamoja na mambo
mengine yanayowazunguka,maana neno lake linasema palipo wawili watatu yeye yupo
katikati yao,upako wa uwingi nao una umuhimu sana.
Unapukuwa
katika maombi ni vizuri pia ukatubu maana unaweza ukawa na vitu vinavyozuia
mawasiliano yako na Mungu. Tubu kwa chochote ambacho umefanya kwa kujua au
kutojua maana Mungu wetu ni mtakatifu uende mbele zake ukiwa mweupe,Amen
2.
Je
wewe ni mtu sahihi au unayefaa kuoa au kuolewa
Kitu
kingine cha kuangalia nafikiri ni vizuri kujifanyia utafiti wewe
mwenyewe,kujichunguza hivi kweli mimi kweli nina tabia gani ya kufaa kuishi na
mtu mwingine. Hivi kweli mimi ninazo tabia za mke au mume mwema kweli ? Hivi
mimi ni mtu ambaye watu wanaweza kumwamini na kumpa moyo wake kweli?
Ni
kwanini nataka kuolewa au kuoa? Nataka kuolewa au kuoa kwasababu mama au baba yangu anahitaji
hivyo,au kwa vile rika langu wote wameolewa? Jamii inanionaje kwanza?
Ukijitafiti
utagundua kwa njia moja au nyingine kuna mtu alishakupa mrudisho nyuma juu ya
tabia zako mbaya,je kwa hizo tabia kweli bila kuzibadilisha kuna mtu anaweza
kuishi na wewe? Jiulize peke yako wala usimuulize mtu,utapata majibu hayo utashangaa
ambavyo unahitaji ujishughulikie kwanza. Watu wengi wanalia katika maombi oooh
Mungu baba Jehova,naomba unipe mtu anayefaa kuwa mume au mke wangu lakini wao
wanasahau hivi mimi Mungu ananionaje,kweli maisha yangu yanampa Mungu utukufu.
Unaweza ukawa na vitabia ambavyo unaona kwamba si vibaya kumbe hivyo hivyo
vyaweza kusimama kama kizingiti cha Baraka zako.
Ukishajua
tatizo liko wapi badilika,saa nyingine kuna watu wanakuja na nia ya kuwa wenzi
halafu wanaingia mitini basi ukijikagua unaona inawezekana tabia hii ndio
imemkimbiza,basin i vizuri kufanyia kazi na sio kukaa na kulia. Kwakweli ni
heri umlilie Mungu atakurehemu kuliko huyo aliyekukimbia maana akishaamua ndio
ameamua na kama sio ubavu wako basi acha aende kwa ubavu wake,amen
3.
Uhusiano
na Mungu
Unapokuwa
unahitaji Mungu akupe mwenzi wako wa maisha pia ni vizuri kujichunguza juu ya
uhusiano wako na Mungu. Je ushirika wako na Mungu uko vipi? Isije ikawa
unakwenda tu kanisani kwasababu unataka Mungu akupe mwenza na wakati hujakaa
sawasawa na huyo Mungu. Hakikisha unajitoa sana kumpenda Mungu na
kujishughulisha na kazi yake yaani utashangaa jinsi mambo yako yatakavyokwenda
bila kuchoka.
Ukijishughulisha
sana na mambo ya Mungu na Mungu naye atajishughulisha na mambo yako.
Kwahiyo
mpendwa chukua hatua leo ya kujitoa kwa Mungu kiujumla sit u kwasababu unataka
mwenzi bali kwa vile umeamua kumpenda Mungu.
Endelea
kututembealea maana ndio kwanza tumeanza,karibu kila wiki kutakuwa na kitu
kipya cha kukusaidia.
Barikiwa
unavyoweka haya katika matendo na tutaomba shuhuda kwa wale mliobarikiwa na
somo hili.
Point nzuri! Point namba nne mabinti wasiangalie hela hasa bongo.
ReplyDeletepoint nyingine: kuwa mwenye bidii kwa kila ufanyacho (halali na venye kumpendeza Mungu) kama dent piga sana shule, kama employee piga sana kazi. hatutaki wachumba au wenza wavivu, wasiojishughulisha wenye visingizio kibao....
ReplyDeletePoints! Nimepata fundisho zaidi, na nadhani kama isha ni cost
ReplyDelete