Thursday, March 21, 2013

Joshua Makondeko Kuzindua Albamu ya" Malipo" Siku ya Jumapili

 
MC na Mwimbaji wa nyimbo za Injili Joshua Makondeko anategemea kuzindua Albamu ya " Malipo" tarehe 24/3/2013,jumapili ijayo. Katika mahojiano Makondeko amesema Albamu ya Malipo itazinduliwa katika DVD na VCD siku hiyo.
Uzinduzi huo utafanyika katika kanisa la City Harvest lililopo Mabibo,Victoria Station( Kituo cha basi cha Garage),kwenye Victoria Building ghorofa ya pili,kuanzia saa 7 mchana.
Na habari Njema zaidi ni kwamba hakuna Kiingilio au kwa kiingereza ni ENTRACE FREE...
Kwahiyo unachotakiwa kuandaa ni hela ya kununua CD yako tu ambazo zitauzwa kwa bei ya punguzo.
Makondeko anazo albamu nyingine 2 a,ambazo ni:
  • Mimi sio Mtumwa
  • Siku za Mwizi Arobaini
 
      Sikiliza Za Mwizi Arobaini Hapa
     
Ya tatu ndio hiyo itakayozinduliwa.
 
Katika uzinduzi huo kutakuwa na waimbaji mbalimbali kama Masanja Mkandamizaji,John Nyuki ,Sifa John na wengine.
 
Zaidi ya uimbaji Makondeko pia ni MC,na pia ana mke ambaye ni mnigeria na wamebarikiwa kuwa na mtoto mmoja.
 
Makondeko anasema anawapenda sana na anawakaribisha wote tuje kumsifu Bwana Yesu kwa pamoja.
 
 
 
 

1 comment:

  1. Ts gonna be hot never happen n all r welcome with much love to you mya fans.......Mc.makondeko.

    ReplyDelete