Tuesday, March 12, 2013

TAFES Associate Nyama Choma Party yawa kichochezi cha kuiendeleza TAFES


Associates wakikaribishwa na wenyeji Mr & Mrs Mramba
 
Mwenyekiti wa Associate Dar,Mr Cuthbeth Simalenga akikaribisha watu

Siku ya Jumapili,TAFES Associates wa Dar es Salaam walikutana nyumbani kwa Associate Felchism Mramba kwa nyama choma. Kwakweli party hiyo ilikuwa ya kufana maana kwanza Associates walianza na supu tofauti na vile tulivyozoea.Ndipo ukafika muda ambao wengi walikuwa wanauongoja wa nyama choma...kwakweli ilikuwa kazi maana watu walifurahia mbuzi choma ambaye alichomwa kwa ustadi.
Kwawale ambao hamkuwepo poleni sana maana associates walifurahi sana hasa kukutana na mates wao wa vyuoni.


Baadhi ya Associates


Kulikuwa na viburudisho vingi zaidi ya chakula kama vile wanakwaya wa zamani kuimba nyimbo walizokuwa wanaimba enzi hizo,huku wakiongozwa na mpiga kinanda wao Amani.

Kwaya ya Zamani ya UCF hiyo
Mrs Rose Mramba akitukaribisha supu...watu weweeeee


Christian Women Bloggers hatuwa mbali

 


 Baada ya kula sasa ikawa ni kukumbushwa majukumu yetu kama associates,kwamba tusije tukakubali kuiacha TAFES iyumbe hasa kifedha maana programme nyingi zinategemea kujitoa kwa associates.Kwakweli TAFES ni taasisi iliyotulea tukiwa chuoni na ilisaidia sana kupanda mbegu isiyoharibika katika maisha yetu,na ndio maana tuko kama tulivyo leo tunasonga mbele na Yesu,Halleluyaaaaaaaaa


Mr Rex,TAFES Director akisisitiza jambo

Kulikuwa na mambo mengi,cha msingi wewe associate mwenzangu usiisahau TAFES kumbuka programme ulizojifunza chuo kupitia TAFES,ujue yuko binti au kijana atafikiwa kwa wewe kuendelea kuisupport TAFES.

Pia katika nyama choma party hiyo mwenyekiti wa bodi TAFES Dr Mbilinyi  alimaliza muda wake na mwenyekiti mpya kusimikwa rasmi ambaye si mwingine bali ni...otea basi Brother Bernard Mono
Brother Bernard Mono,Mwenyekiti mpya wa Bodi ya TAFES
 

Mungu atusaidie wapendwa katika Bwana,tuweze kuiendeleza TAFES yetu.Amen


2 comments: