Wednesday, March 6, 2013

Mchungaji Lilian Ndegi:Wanawake wajiandae kupokea urejesho wa mioyo yao kupitia Kongomano la Moyo wa Mwanamke 2013


 
Maneno hayo aliyasema Mchungaji Lilian Ndegi ambaye ndio mbeba maono ya “Moyo wa Mwanamke”

Katika mahojiano tuliyoyafanya alisema kwamba “Moyo wa Mwanamke ni maono yamepandikizwa ndani yangu na Roho Mtakatifu.

Na Makongomano ya Moyo wa Mwanamke yalianza mwaka 2008 na la kwanza lilikuwa na wanawake takriban 2000, makongomano hayo yanafanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya mwezi wa 3.Target ni kila mwanamke yoyote aliyeokoka na asiyeokoka,yoyote,kaunzia mabinti hadi wabibi.

Lengo kubwa ni kuweka kitu cha ki MUNGU kitakachamfanya mwanamke aishi maisha ya ushindi hapa duniani? Halleluya!
Mchungaji Lilian Ndegi katika huduma

Alipoulizwa ni Kwanini wanawake tu na sio wanaume Mchungaji Lilian Ndegi alisema”mzigo aliopewa ni wa wanawake sio kwamba ana uchaguzi. Ila wanaume wanaweza kuja maana Neno la Mungu linapotoka linafanya kazi kwa mtu yoyote,japo utakuwa ujumbe wa wanawake lakini mwanaume akija anaweza kupata ujumbe wake nae.

Somo hasa watakalofundisha yeye na watumishi wengine linalohusu Moyo wa Mwanamke,kuna nini? Atajua moyoni mwake kuna nini? Na ajihoji alichonacho ni kitu sahihi? Ajue mambo anayopitia magumu yote yanatokana na kile alichokibeba moyoni, na tutakuwa tunafundisha kwa ajili ya kutoa kitu dhaifu na kupanda kitu Mungu alichokipanda.

Hili Kongomano litakuwa la Mafundisho zaidi si la maombezi,japo tutaombea watu ila mafundisho ndio zaidi.

Mchungaji Lilian Ndegi aliendelea kusema kwamba Ukienda nyumba za maombezi, au kwa waganga wa kienyeji,mahospitali wengi utakaowakuta huko ni wanawake,hapo ndio akatafuta nini kiini,akataka kujua chanzo ni nini, kwahiyo Roho Mtakatifu amemwezesha kwenda kwenye shina la tatizo. Ambapo ndio kwenye uponyaji wa Moyo wa Mwanamke.

Mwanamke akipona moyo atapata urejesho wa yale yote yanayomsumbua katika maisha yake maana wanawake wengi wana mapito mbalimbali katika ndoa zao,kazi,biashara,mashuleni na kila mahali.

Makongomano yaliyopita yalifanyika kwa siku moja ya ijumaa tu,halafu wakaongeza ikawa siku2, na Mwaka huu ni kuanzia ijumaa hadi jumapili.

Kwa kupitia makongomano yaliyopita wamepata shuhuda nyingi,wanawake wengi wamejitambua na wanaishi maisha ya raha ya kujitambua,pia wengi wamepata uponyaji wa miili kama kupona ulcers,Pressure,Mifupa etc vinavyoletwa na stress walizonazokuwa nazo

Watumishi watakaofundisha siku hiyo ni Pastor Lilian  Ndegii Pastor Naomi Mhamba na Pastor Grace Kapswara kutoka Zimbambwe.

Kiingilio ni Bure Kabisa labda utayari wa moyo wako ndio muhimu sana,maana tunatamani wanawake waondoke wakiwa wamebadilishwa na kluponywa mioyo yao.

Muda : Saa 3 asubuhi hadi 11 jioni.

Waimbaji na vikundi mbalimbali vitahudumu na kuburudisha;Upendo Nkone,Madam Ruth,Praise n Worship,vikundi mbalimbali,waimbaji mmojammoja wengi

Siku za Kongomano ni Tarehe  8,9,10 Mwezi wa Tatu

Mchungaji Lilian Ndegi anawakaribisha wanawake wote  waje maana Mungu ana kitu kipya kwa watu kila wakati


Haya Haya wanawake wenzangu tujitahidi tukajifunze...
 

 

1 comment:

  1. Good post. I learn something new and challenging on websites I
    stumbleupon on a daily basis. It's always interesting to read through articles from other writers and practice something from their web sites.

    Here is my website - .UTTVLzDqh8E
    My web site :: predictions that came true

    ReplyDelete