Rev Florian Katunzi |
Karibuni katika makala haya yanayofundishwa na Mchungaji Florian Katunzi wa Kanisa la EAGT City Centre lililopo katika viwanja vya Sabasaba.
Endelea........
*1Samweli
17: 39-50
*“ Daudi
akaichukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe laini matano katika kijiti
cha maji, akayatia katika mfuko wa kichungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake
na kombeo lake alilokuwa nalo mkononi mwake”.
Daudi
anamshinda Goliathi, sauli na majeshi yake walishindwa kumpiga Goliathi,
maandiko yanathibitisha silaha za daudi ni kama ifuatavyo.
- Fimbo
kiblia inawakilisha mamlaka katika mfufulizo wa mateso yetu, nataka
nikufundishe juu ya mawe matano.Daudi aliyoyaweka kwenye kifuko chake cha kichungaji kabla ya
kumpiga Goliathi, pia kwa nini yawe mawe matano na si sita wala saba. Katika
maisha ya kiimani lazima kuwepo msingi wake ndipo mtu wa Mungu anapoweza
akajenga anayotaka kujenga.
- Jiwe
la kwanza la kumfanya mtu wa Mungu ajijenge ili pate kutokutikisika kama vile
Daudi ambavyo hakuyumba wala kuogopa,
maana alijua alicho nacho ndani ya mfuko wake kina uwezo katika Mungu hata
kuangusha ngome za adui shetani katika ulimwengu wa roho.
-JIWE LA
KWANZA: *NI NENO
*Yohana
1:1-5 * “ Hapo mwanzo kuliwako neno naye neno alikuwako kwa Mungu, naye ni neno
alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu, vyote vilifanyika kwa huyo wala
pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa
uzima nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru ya ng’aa gizani, wala giza
halikuiweza.”
- Nataka
tujifunze na tuione jinsi ambavyo jiwe hili la kwanza ambalo ni NENO lilivyo na
nguvu ya kuangusha kila silaha za adui, hivyo ushindi wa Daudi ulitegemea mawe
matano kuwa ndani ya mfuko wake, pasipo NENO hakuna kilichofanyika wala
kitachofanyika katika maisha yetu ya kiimani. NENO la Mungu linaleta uzima
kwake yeye atayeliamini , kabla ya yote palikuwapo NENO na yote yakawepo tunayoyaona ya mbinguni
na duniani.
-
A. NENO LINAUMBA.* Zaburi 33 : 6 – 9
“Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa
chake maana yeye alisema ikawa nay eye aliamuru ikasimama.”
*
Waibrania 11: 3 “ Kwa Imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa Neno la
Mungu, hata vitu vinayoonekana, havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.”
-Lazima
mtu wa Mungu ufahamu kabisa pasipo kulishika Neno, kulitimiza Neno, kulikamata
Neno na kulitii Neno la Mungu uto weza kushinda vita vya kiroho wala kuziona
baraka za Mungu zilizomo katika Neno lake, kabla ya mambo yote kwanza ujue neno
la Mungu.
-B. NENO
HUTAKASA.* Yohana 15 : 3 “ Ninyi mmekuwa safi kwasababu ya Neno nililowaambia.”
-
C. NENO LA MUNGU NI TAA YA TUMAINI. *
Zaburi 119: 105 “ Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu.”
-D. NENO
NI NURU. Kwa yeyote atakayelishika
hatawenda gizani, * Zaburi 119:130 “Kufafannusha maneno yako kwatia nuru, na
kumfahamisha mjinga.”
-E. NENO
LA MUNGU NI UPANGA WA ROHO * Waefeso 6:17 “ Tena ipokeeni chepeo ya wakovu na
upanga wa roho ambao ni neno la Mungu”
Upanga
wa Roho ni silaha ya muumini (mkristo) ambayo anapaswa kuitumia kwenye vita vya
kiroho dhidi ya silaha za uovu za shetani. Lakini pia ujasiri wetu humo katika
neno tunaona Yesu kristo alivyotumia upanga wa roho kumshinda shetani. Hili ni
jiwe la muhimu sana katika maisha ya watu waliokoka yaliyojaa vita.
Ukisoma
katika kitabu cha Luka 4:1-13, utaona pamoja na kuwa Yesu alikuwa amejaa Roho
Mtakatifu bado shetani alimjaribu kwa kupanga vita mbele yake kwa kutumia jiwe
la neno na Yesu pia alitumia jiwe hilohilo kumnshinda shetani.
Hivyo
kama mkristo aliyeokoka anapaswa kuwa makini na maneno yote yanayokuwa
yanatamkwa kinyume dhidi yake kwa
kuyabatilisha au kuyatengua kwa jina la Yesu. Ukiangalia kwa undani zaidi
utagundua kuwa wakristo wengi wananaswa na mitego ya shetani kwa kutokujua neno
la Mungu na uweza wake.
1Samweli
17:1-58, inaonesha kuwa wakati Sauli anamwambia Daudi kuwa hawezi kumshinda
Goriathi kwasababu ni mtu wa vita tangu siku nyingi, katika hali halisi ya nje
Daudi asingeweza kupigana na Goliathi lakini Daudi alijua neno la Mungu na
ndilo lililomsaidia.
Yoshua
1:5, “Hapatakuwa na mtu yoyote atakayeweza kusimama mbele yako, siku zote za
maisha yako kama nilivyokuwa na Musa ndivyo nikatavyokuwa pamoja na wewe,
sitapungukia wala sitakuacha”
Wakati
mfalme anatetemekea na kuangalia ukuu wa Goliathi, Daudi yeye anaangalia ukuu
wake Yehova mwenye nguvu. Lakini pia wakati watu wanatazama mapungufu ya
mwanadamu Mungu yeye hutazama uwezo wake mwanadamu huyo katika kumtumikia.
Wafilipi
4:13, “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”
2Wakoritho
10:3-4, “Maana ingawa tunaenenda katika mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili
, maana silaha za vita vyetu si za mwili bali zinauwezo katika Mungu hata
kuangusha ngome”
F. NENO
LA MUNGU NI HAI TENA LINA NGUVU KATIKA MUNGU.
Waebrania
4;12-13, “ Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu , tena lina ukali kuliko
upanga likatalo kuwili , tena linachoma kuzigawanya nafsi na Roho, na viungo na
mafuta yaliyomo ndani yake , tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya
moyo wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake; lakini vitu vyote vi utupu
na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”
Tunajifunza
kuwa neno la Mungu ni muhimu sana hasa katika imani na hata tunapoomba maombi
ya ulinzi lazima kwanza mtu ajue neno la Mungu. Mwanafunzi mzuri wa Yesu Kristo
lazima akae katika neno la Mungu.
Yohana
8:31-32, “ Ninyi mkikaa katika neno la Mungu mmekuwa wanafunzi wangu kwelikweli
tena mtaifahamu kweli itawaweka huru”
Kweli ya
Mungu imo ndani ya neno lake , lakini wakristo wengi wa leo wanadanganywa na
watu wanaotumia mapepo ya utambuzi au roho za utambuzi wakidhani ni
manabii.Hali hii inapelekea kanisa kudanganywa katika kiwango kikubwa.
Habari
za mapepo ya uaguzi zinapatikana katika kitabu cha 1samweli 28:4-25, ambapo
inaonyesha jinsi mfalme Sauli alipoacha kushika neno na kulifuata , akaanza
kufuata njia za uganga maana Mungu hakuwa amemjibu maombi yake. Ukiendelea kusoma utagundua jinsi nguvu ya
utambuzi ilivyomsaidia mfalme Sauli
kupata majibu aliyoyataka maana shetani alijigeuza kuwa malaika wa nuru.
Wakristo
wengi wametekwa na Roho zidanganyazo ili mradi wameelezwa habari zao za siri
ambazo hata hizo zinafanyika v ilevile kwa waganga wa kienyeji.
Kumbukumbu
12:1-11, katika sura hii biblia inaelezea kwa ndani zaidi kuzuka kwa manabii
wengi wa uongo na waotaji ndoto , wakitolea ishara ya mambo yajayo. Hivyo
wakristo wanapaswa kuwa na misimamo na kuacha kushawishika na hao waota ndoto
na ishara zao kwani jambo ambalo lin aweza kuleta mahusiano mazuri baina ya
Mungu na mwanadamu si katika ishara na maajabu.
1Yohana
4:1, “ Wapenzi msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho , kwamba
zimetokana na Mungu kwasababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”
Watu wa
namna hii wanaweza wakazungumza katika upako wa kipepo na ukadhani ni wa
kimungu , watatabiri kwa usahihi mambo yajayo
na kutenda miujiza na maajabu yakatenda, maandiko hayajasema hawatatenda
(ishara) Yesu kristo anasema;
Mathayo
24:11, “na manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi”
Marko
13: 22, “ Kwa maana wataondoka makristo wengi wa uongo , na manabii wa uongo
watatoa ishara na maajabu wapate kuwadanganya kama yamkini hata wao wateule”
Yesu
kristo analionya kanisa kuwa macho na
wapotoshaji wa kweli ya Mungu. Na kulitahadharisha kuwa pasipo kujua kweli ya
Mungu waklristo wengi watanaswa na roho hizi zipotoshazo.
Mathayo 7:15-17”Jiadhari na manabii wa uongo , watu
wanaowajia wavaa mavazi ya kondoo walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali.
Mtawatambua kwa matendo yao , Je, watu huchuma dhabibu katika miiba au tini katika mibamiti vivyo hivyo mti mwem
ahuzaa matunda mazuri na mti mwovu huzaa matunda mabaya”.
Yesu
anasema wazi kuwa pasipo kujua neno basi itakuwa ngumu sana kwa mkristo
kuzishinda hila za mwovu shetani. Anaongeza kwa kuonya kuwa,
Mathayo
7:21-23, “Si kila aniambiaye BWANABWANA atakanyaga katika ufalme wa mbinguni
bali yeye afanyaye mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni wengi wataniambia siku
ile BWANABWANA hatukufanya unabii kwa jina lako , kutoa pepo kwa jina lako,
kufanya miujiza mingi kwa jina lako, ndipo nitawaaambia dhahiri sikuwajua ninyi
kamwe , ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu”
Wakisto
wengi katika maisha ya sasa wamekuwa wakipenda zaidi miujiza na hata kupelekea
kukimbilia katika ibada za watu wafanyao miujiza, hata hivyo bado maisha ya
wakristo wengi ni machafu kwani mlevi,mzinzi,mchawi, na hata wavaa hirizi nao
pia wanataka miujiza. Lakini ukweli ni kuwa hakuna muujiza kwa mtu ambaye
ameambatana na uovu katika maisha yake.
Zaburi
103: 3-5, “Akusamehe maovu yako, akuponya magonjwa yako yote, atakomboa uhai
wako na kaburi, akutia taji ya fadhili na rehema, akushibisha mema uzee na
maisha yako yote.
Mambo
haya yote yatakuwea juu ya mwanadamu pindi atakapotubu dhambi na kuziacha.
Isaya
3:10-11, “ Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maaana watakula
matunda ya matendo yao. Ole wake mtu mbaya , shari itakuwa kwake kwa maana
atapewa ijara ya mikono yake”
Dhambi
ni kikwazo kikuukwa mtu yoyote ambaye anahitaji msaada wa kimungu ndio maana
wapo wakristo wengi ambao wanashida mbalimbali na wanazunguka katika makanisa
mbalimbali wakitafuta maombezi lakini hawafunguliwi kutokana na mizigo ya
dhambi waliyonayo.
Kutii
neno kwafaa sana maana huondoa magonjwa na vifungo mbalimbali ambapo katika
neno la uponyaji na ulinzi Kutoka 23:22-26, “ Lakini ukilisikiza sauti yake
kweli na kuyatenda yote ninenayo mimi, ndipo mimi na mtesi wa hao wakutosao kwa
kuwa malaika wangu atakutangulia mbele yako, nanyi mtamtumikia Bwana Mungu wenu
, naye atawabarikia chakula chako na
maji yako, nami nitakuondolea ugonjwa kati yako, hapatakuwa na mwenye kuharibu
mimba wala aliye tasa katika nchi yako na hesabu ya siku zako zitazitimiza”
Kutii
neno pia kunaleta ulizi na baraka Matendo 28:1-14
Pasipo
kutii neno la Mungu hauwezi kubarikiwa
Mithali 12:11, “ Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele bali
afuataye mambo ya upuuzi hana ufahamu”
Mitahali
10:14, “ Atendaye mambo kwa mkono legevu huwa masikini, bali mkono wake aliye
na bidii hutajirisha”
Mithali
19:15, “ Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito na nafsi yake mvivu itaona
njaa”
Mithali
20:13, “ Usipende usingizi usije ukawa masikini”
Kimsingi
umasikini hauwezi kuondoka kwa maombi peke yake bali kwa kujituma kwa bidii
sambamba na kulifuata neno.
No comments:
Post a Comment