Kanisa la Olasiti lililolipuliwa |
Kwa hisani ya Wavuti........
UPDATE/TAARIFA MPYA
· Kijana mmoja anashikiliwa na Polisi kama mshukiwa wa mlipuko huo (inadaiwa alipokamatwa alikutwa na stock nyingine ya mabomu)
· Mtu mmoja amefariki (mwanakwaya)
· Waliojeruhiwa jumla ni 66.
Majina ya waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospitali za
maunt Meru, na hospitali teule ya jiji la Arusha ya St Elizabeth wametambulika
kuwa ni:- John Thadei, Regina Fredirick, Joram Kisera, Novelt
John, Rose Pius, John James, Anna Kessy, Joan
Temba, Neema Kihisu, Gloria Tesha, Innocent Charles, Fatuma
Haji, Fikiri Keya, Simon Andrew, Anna Edward, Lioba
Oswald, Rose Pius, Philemon Gereza, Kisesa Mbaga na Beata
Cornell.
Majeruhi wengine na umri wao katika mabano, ni Consensia Mbaga (53), Christopher
Raymond (10), Deborah Joachim (24), Elizabeth Isidori (24), Anna
Didas (52), Bertha Cosinery (49), Edda Ndowo (77), Derick
Cyprian (8), Faustine Andrea (35), Mary Okech, Mesoit
Siriri (33), Clenes pius (22), Joyce yohana (15), Restituta
Alex (50), Mathias Riha (74), Magreth Andrew(45), James
Gabriel (16), Regina James (17), Elizabeth Masawe(15), Elizabeth
Sauli (18), Njau (35), Yasinta Msafiri (16) Doreen Pancras
(28), Alex Arnold, Agripina Alex (9), James Gabriel (16), Loveness
Nelson (17), Amalone Pius (25), Frank Donatus (10), Alphonce
Nyalandu (26), Athanasia Reginald (14), Phillemon Ceressa (49), Neema
Daud (13), Sophia Kanda (72), Theofrida Innocent (21) na Regina
Darnes(17).
UPDATE/TAARIFA MPYA saa 12:47 mchana
1. Baba Askofu Mkuu wa Jimbo la Kanisa Katoliki
Arusha, Mhashamu Josephat Louis Lebulu na Mwakilishi wa Papa, Nuncio, Francisco
Montecillo Padilla wameondoshwa katika eneo la tukio na kikosi cha ulinzi na
usalama.
2. Kikao cha dharura cha ulinzi na usalama kimeafikiana
kusitisha shughuli ya leo hadi hapo itakapotangazwa upya.
3. Padre Simon Mtengesi amefunga rasmi ibada kwa
sala fupi na kuwaomba watu warejee majumbani mwao.
4. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo amefika
na kutizama maeneo ya Kanisa, kisha akazungumza kwa kusema kuwa mwakilishi wa
Papa alikuwepo Arusha tangu tarehe 2 Mei mwaka huu akitembelea maeneo kadhaa ya
mkoa huo, ikiwemo Ngorongoro na leo akiwa katika kilele cha ziara yake kwa
kuzindua Parokia mpya, ndipo mlipuko huo ukatokea na kusababisha shughuli nzima
kuahirishwa. Mulongo amesema wataalamu wa uchunguzi kutoka Makao Makuu ya Jeshi
la Polisi wanatarajiwa kuwasili mkoani Arusha kuungana na kikosi cha Mkoani
hapo ili kufanya shughuli ya uchunguzi.
5. Mkuu wa kikosi cha Polisi cha usalama Mkoani Arusha,
RPC Kamanda Liberatus Sabas amefika katika eneo husika na kuzungumza akisema
kuwa walipokea taarifa za tukio kwa maelezo kuwa mlipuko ulitokana na kitu cha
kurushwa kutoka kwa mtu mmoja aliyefika eneo hilo kwa gari. Hadi sasa Polisi
inamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano zaidi na inaomba wananchi wenye
taarifa zaidi waziwasilishe katika vyombo husika.
6. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefika
katika eneo na kuzungumza na wananachi. Amesema hili ni tukio la kushitua sana
kwa kuwa limetokea kwenye eneo la ibada, wakati misa ikiendelea... (mawasiliano
ya redio yamekatika wakati Lema anazingumza. Baada ya muda mtangazaji wa Radio
Maria ameomba samahani kuwa kuna mtu alizima swichi. Baadaye mwandishi alimpata
Lema akiwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jashua Nassari na kuwapa nafasi ya
kuzungumza na kutoa ujumbe wao kwa wananchi.) Baadaye Lema na Nassari
walikwenda hospitalini na kujitolea damu na kuhamasisha vijana kufanya hivyo,
zoezi ambalo waliliunga mkono na kuanza kushiriki.
7. Padre wa Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu,
Sombetini katika Jimbo Kuu la Arusha, Moses Mwaniki amewapa pole majeruhi na
kuwaomba watu kujitolea kwa maji na vyakula kwa ajili ya kuwajali majeruhi
zaidi ya 30 waliolazwa katika hospitali mbalimbali za ndani na nje ya mkoa
huo.
---
Mwendo wa kuelekea saa tano adhuhuri ya leo katika iliyokuwa iwe Parokia ya
Mpya ya Yosefu Mfanyakazi iliyokuwa inafunguliwa leo, pametokea mlipuko
uliojeruhi watu kadhaa, watatu wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana.
Kwa mujibu wa taarifa zinazosikika moja kwa moja kupitia Radio Maria, Tanzania,
mlipuko huo umetokana na kitu ambacho kinasadikika kuwa lilikuwa ni bomu. Hata
na hivyo haijafahamika ikiwa kama ndivyo, lilikuwa ni bomu la kutegwa ama
kurushwa kwa mkono. Ni vigumu na mapema sana kuthibitisha kilicholipuka.
Tafadhali tuvute subira kwa kuisubiri taarifa ya Polisi.
Inaripotiwa kuwa wengi wamejeruhiwa miguuni na kulazimika kuwahishwa
hospitalini kwa matibabu zaidi. Hakuna taarifa zozote za kifo zilizoripotiwa.
Majeruhi wamepelekwa katika hospitali mbalimbali za mkoa huo kwa matibabu
zaidi.
Kwa muda huu, viongozi mbalimbali wa Kanisa akiwemo mwakilishi wa Papa
aliyekuwa anatabaruku Kigango hicho kilichozaliwa mwaka 2008 kuwa Parokia,
Nuncio, Francisco Padilla na viongozi wa jeshi la polisi na usalama,
wanaendelea na kikao ili kuamua hatima ya misa iliyokatizwa.
Hizi ni taarifa za awali tu, kwa ajili ya kukupasha kinachoripotiwa redioni.
Taarifa kamili itawekwa itakapopatikana. Tafadhali endelea kusikiliza Redio
Maria Tanzania (inasikika pia online, tizama kwenye menu ya Redio hapo juu) muda huu
wakiwa wanatangaza kuhusu tukio hili.
No comments:
Post a Comment