Watarajiwa...... |
Leo tunaendelea na somo letu la tano juu ya vitu muhimu vya kuangalia unapotafuta au kijuandaa kuwa na mwenzi wa maisha.
Tunapoendelea na somo hili ambalo ni pan
asana,tumelichambua vizuri sana tukiangalia vitu muhimu ambavyo mhusika
anayetegemea kupata au kutafuta mwenzi anatakiwa ahakikishe anavifanyia
kazi,halafu tuliendelea kuangalia sasa vitu gani muhimu uangalie kwa huyo
anategemea kuwa mwenzi wako.
Hivi vipengele ni muhimu sana kwa wewe ambaye
unategemea kuingia kwenye ndoa na pia hata kwa mwanandoa maana vitakusaidia
kutengeneza kwa upya juu ya ndoa yako.
Ni maombi yangu somo hili likawe Baraka na kukupeleka
katika lile kusudi ambalo Mungu analo juu yako juu ya mambo ya ndoa.
Tuendelee..
3. Je huyo
mtu anakupenda kwa dhati
Ni muhimu sana kuwa na uhakika wa kiasi cha upendo alichonacho mtarajiwa wako. Mwingine
anaweza kuwa na wewe kwasababu tu labda amevutiwa na umbile au vitu ulivyo
navyo.
Kuna mpendwa mmoja aliingia kwenye uhusiano akifikiri
kwamba huyo mtarajiwa anampenda,basin a yeye akajitoa san asana kwake,kumbe
yule mtarajiwa alikuwa tu anapenda kuwa na yule mpendwa kwasababu alikuwa ana uwezo wa kifedha. Sasa
hii ilikwenda hivyo ila kitu kizuri ni kwamba yule mpendwa alikuwa na mahusiano
mazuri na Mungu wake,basi akawa anaendelea kumuomba Mungu juu ya ule uhusiano
ndipo siku akaja kugundua kwamba yule mpendwa ana mahusiano na mtu mwingine
ambaye sasa ndio anayempenda ila yeye alikuwa anamtumia tu kwasababu ana hela.
Ashukuriwe Mungu maana hakuruhusu waingine katika ndoa,maana angeteseka sana
huyo mpendwa kuwa na mahusiano na mke au mume ambaye hakupendi.
Nimetoa ushuhuda huu kukupa tahadhari na kukuonyesha umuhimu
wa kuwa na mahusiano na Mungu kama nilivyokwisha kutoa somo hapo Nyuma.
a. Kuweza
kuchuliana katika madhaifu
Unatakiwa ujue kwamba hakuna mwanadamu aliyekamilika
hapa duniani kila mtu ana madhaifu yake,sasa kama mtu hana upendo wa kweli
itakuwa ngumu sana kwake kumchukulia mwenzake.
Maneno ya Mungu katika Waraka wa Kwanza wa Petro 4:8
inasema “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu
upendano husitiri wingi wa dhambi”
Mtu akiwa na upendo ataweza kuvumilia pale mwenzake
anapokosea na akamsamehe kabisa,lakini akiwa hana upendo hatamsamehe.
Upendo utakuwezesha usimuhumu mwenzako kwa historia
yake ya nyuma kama alikuwekea wazi,kwa mfano kama mtu kabla ya kuanza mahusinao
akamwambia mwenzake kwamba nina mtoto au huko nyuma nilikuwa na a,b,c,ukiwa na
upendo utamsamehe lakini wengine ndio kwanza anakukimbia na anakuwa na kazi
moja tu ya kukutangaza labda kwenye kanisa ooh mnamuona yule yukom hivi na vile
ooh unajua ana watoto watano tena baba tofauti ooh unamuona yule alikuwaga na
mahusiano a,b,c ,unamuona yule alishavutaga bangi. Hapo utakachokuwa unakifanya
ni kumuumiza mwenzako na sio kumsaidia,lakini ukiwa na upendo utamuombea na
utamtia moyo wa kusimama Imara na Yesu.
Au kuna ushuhuda mwingine naujua huyo mtu alioa mdada
ana mtoto wakaishi vizuri kipindi cha mwanzoni ,yule mama alivyopata watoto
wengine wa yule baba, yule baba akaanza kuwabagua yaani mwisho alimkataa kabisa
yule mtoto wa yule mama. Hapo ina maanisha hakuwa na upendo wa kweli na yule
mama ndio maana akashindwa kumchukulia na mambo yake.
Kwahiyo mpendwa kuwa makini na huyo mtarajiwa msome
vizuri sana asije akawa anakubali vitu vyako kumbe tu anataka aingie tu kwenye
ndoa.
Upendo unawaunganisha kuwa na mamoja na kuwa na nia
moja.
Pasipokuwa na upendo hata umoja wa wanandoa unakuwa
haupo. Utakuta mtu hata hajui mwenzi wake kaenda wapi au ana tatizo gani.
Katika ndoa ni vyema kushirikiana na kujua hata
changamoto ambazo mwenzako anazipitia na kumuombea,yaani kuichukua shida
mwenzako kama yako.
Maneno ya Mungu katika Kitabu cha Warumi 13:8 “Msiwe na
deni kwa mtu yeyote, isipokuwa tu deni la kupendana. Ampendaye jirani yake
ameitekeleza Sheria”
Upendo ni amri kutoka kwa Mungu,kwahiyo hakikisha
unampendwa mtarajiwa au mwenzi wako.
Mkiwa na Upendo,mtakuwa mnaomba pamoja na kusoma neno
pamoja
Na Mungu atakuwa pamoja nanyi na kwa umoja wenu
mtamshinda Ibilisi na hila zake,maana Ibilisi anapenda mafarakano ili apitishe
mambo yake.
Chukua hatua kama unaona huna upendo wa dhati kwa
mtarajiwa wako jiangalie kwa upya na pia kama mtarajiwa wako hana upendo wa
dhati na wewe yakupasa kukaa chini na kufikiria kwa Upya.
Jina la Bwana libarikiwe.
ushauri mzuri sitalikosa hili somo kila siku asanteni sana
ReplyDelete