Profesa Elisante Ole Gabriel Mkurugenzi Mkuu Idara ya Mendeleo ya Vijana Tanzania |
Maneno
hayo yalisemwa na Profesa Elisante Ole Gabriel ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa
maendeleao ya Vijana katika Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo
alipokuwa anaeleza Vijana juu ya Sera ya Maendeleo ya Vijana katika Ukumbi wa
Nchi ya Ahadi ( The Promise Land). Semina hiyo ni mojawapo ya semina na
mikutano ambayo imekuwa ikifanyika katika ukumbi huo kila wiki ili kuhamasisha
vijana watanzania waweze kubadili mtazamo na kuikwamua nchi yao,mikutano hiyo
inaandaliwa na Mchungaji, MC Maarufu na Mtangazaji wa Redio Clouds FM Harris
Kapiga.
Katika
mkutano huo Profesa Elisante aliwataka vijana wa kitanzania kuachana na dhana
potofu kwamba maendeleo yanahitaji kuwa na mtaji au hela tu wakati tatizo kubwa
liko katika fikra na mtazamo wa vijana kwa ujumla.
Aliendelea
kusema kwamba wameweza kugundua kwamba vijana watanzania wanakabiliana na
changamoto kuu nne; ambazo ni
·
Fikra,kwamba
kuna watu wenye fikra Kubwa,fikra ya wastani na fikra ndogo
Ili
kujikwamua ni lazima vijana waamue kuwa na fikra Kubwa.
·
Uelewa
wa kuongeza thamani katika shughuli za Uzalishaji Mali (Value Addition)
·
Upatikanaji
wa Mtaji kwa gharama nafuu
·
Mifumo
ya kiutendaji kama leseni,lugha,rushwa e.t.c
Pia
aliweza kuelezea jinsi ambavyo serikali imefanya jitihada kubwa kuweza
kupambana na changamoto hizo;
·
Kuanzisha
kanzidata ya taarifa za Vijana ili kujua takwimu ya vijana ikoje,kwa mfano
wangapi wana kazi wangapi hawana
·
Kuzungumza
na Taasisi za fedha ili kupata mikopo ya gharama nafuu
·
Kuimarisha
mfuko wa maendeleo ya vijana ili kuwezesha vijana kupata mikopo ya vikundi kwa
gharama nafuu
Alielezea
pia mambo ya msingi kwa vijana yanayoweza kuwezesha Sera ya Maendeleao ya
Vijana kutekelezeka kwa urahisi
·
Vijana
wasibaguane kwa rangi,dini,siasa,jinsia,jiografia,elimu,kipato au tofauti
yoyote ile
·
Kijana
awe na itikadi ya dini na siasa ila ujana wako usiwe na itikadi
·
Vijana
wafanye kazi kuanzia asubuhi,hapa akasema tatizo vijana wengi wanalala sana
·
Kila
mtu ahuheshimu ujana wako,pia wewe ujiheshimu ili uheshimiwe
Harris Kapiga Mchungaji,Mc na Mtangazaji mwenye mzigo na Vijana wa Ktanzania |
Kwa
kweli semina hiyo ilikuwa nzuri sana iliweza kuwafungua vijana kujua hata fursa
ambazo wanazo kupitia wizara yao. Na vijana waliweza kuuliza maswali na
kupatiwa majibu pia hata sehemu za kupata huduma katika wilaya zao.
Vijana
walifurahishwa sana na jinsi Prof Elisante alivyotumia muda wake na kueleza kwa
kina na hata akitumia mifano ya maisha yake hadi hapo alipofika aliwapa vijana
changamoto ya kujituma zaidi na zaidi.
Blog
inamshukuru sana Profesa Elisante kwa alivyojitoa kwa vijana na pia inampongeza
sana Harris Kapiga kwa mbegu anayoipanda kwa Vijana wa kitanzania,hasa ile
passion aliyo nayo kwamba Kijana wa Tanzania inawezekana hata kama uko stage
gani.
No comments:
Post a Comment