Usikate Tamaa |
Nawasalimia katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo,
Leo nina ujumbe mfupi kwako wewe ambaye una mzigo
mzitoo sana,umelia sana ,umekata
tamaa,labda huna school fees ya watoto,au hujabahatika kupata mtoto,au hujapata
kazi,au watu hawakupendi wamekuzushia mambo mabaya,au unaumwa ugonjwa ambao
Daktari amesema kwamba hakuna tiba,au unatamani kuwa na mwezi wako wa maisha na
unaona kama muda umeenda,au una
msukosuko katika ndoa mambo sio shwari,au umeachwa mpendwa wangu,au kila
uanchofanya hufanikiwi umejaribu kila biashara na kila fursa haufanikiwi kila
unachoshika na mkono wako kimezaa mapooza matokeo yake vimekuacha katika
madeni, mpendwa natanguliza Pole lakini siku ya leo napenda kukuambia hivi
Bwana Yesu alisema katika 1Peter 5: 7 Neno
katika tafsiri ya NIV "Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye
anawatunzeni",hilo jambo ambalo unaliona Zito sana kwako mtwike Yesu na
yeye atakutunza na kukupumzisha na masumbuko ya dunia hii.
Yawezekana umelia sana sana umepita vituo mbalimbali vya maombi,nakushauri leo mpendwa tulia kwa Bwana na kama neno linavyosema katika Yohana 14:1 "Yesu aliwaambia, "Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia". Yawezekana hata umesafiri nchi mbalimbali kwa watumishi wakubwa ukitafuta suluhu ya kilio chako,lakini umejikuta uko palepale..
Usifadhaike mpendwa liko tumaini,mwamini Mungu kwamba
atafanya katika wakati ambao hukujua utamshangaa Bwana. Mungu anakwenda
kukushangaza (Surprise) nao waliokucheka,waliokata tamaa wakaona kwamba wewe
ndio basi au kukukebehi watajua kwamba unamtumikia Bwana Mwenye uwezo kuliko kitu
chochote duniani na Mbinguni. Mungu anakwenda kukufunika na utukufu wake. Amen
Tena anasema katika Wafilipi 4:6-7 "Msifadhaike
juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa
kusali na kuomba pamoja na kushu kuru 7. Na amani ya Mungu, ambayo inapita
ufahamu wote, italinda mioyo yenu na nia zenu kwa Kristo Yesu"
Unapokuwa katika majaribu usimtafute mwanadamu wa
kukusaidia,wengine wanakimbilia wazazi wao na kuamini ndio watakao wasaidia ni
kweli nafasi ya mzazi ni kubwa lakini atakupa tumaini la muda ,Mungu ndie
mwenye tumaini la kweli na yeye ndio anayekujua kwasababu alikuumba kwahiyo
anayo majibu juu ya maisha yako,anayo majibu juu ya afya yako,anayo majibu juu
mapito yote unayopitia,Songa mbele mpendwa utayapita tuu,nakuambia utacheka
tena mpendwa,utainuliwa,kila kilichokuwa kimeibiwa na Ibilisi katika maisha
yako kitarudishwa kwako,Halleluya
Napenda sana haya maneno katika Yakobo 1:2-4 ” Ndugu
wapendwa, mnapopatwa na majaribu mbalimbali, yahesabuni kuwa ni furaha tupu. 3 Kwa
maana mnafahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu hujenga ustahimilivu. 4 Na
ustahimilivu ukimaliza kazi yake mtakuwa wakamilifu pasipo kupungukiwa na cho
chote.”
Kwahiyo mpendwa ujue kabisa kwa kila jaribu unalipitia
hebu hesabu kwamba ni furaha maana unajengwa,unakwenda kubadilishiwa jina,Mungu
anakwenda kukurejeshea heshima yako,inawezekana umekosa kibali ofisini kwako,au
umeshushiwa heshima na jamii,lakini hebu leo chukua hatua ya Imani na mimi
kwamba ni furaha tu maana Mungu anakwenda kukuvalisha vazi la
Sifa,Halleluya,Jina la Bwana Libarikiwe
Naongea na mtu wakati huu,Usikate tamaa,narudia usikate
tamaa,maana ukishapita kipindi hiki kama neno linavyosema hutapungukiwa na
CHOCHOTE, Amen
Kwahiyo sasa nakusihi wewe ambaye unapita katika
majaribu futa machozi,simama,tembea songa mbele endelea na safari maana
kuanguka sio mwisho wa safari mpendwa wangu.
Kwakweli leo nimekuja kukutia moyo tu na kukupa Ujumbe
Mzuri kwamba Mwokozi wetu Yesu anaweza na atakuwezesha tena,USIKATE
TAMAA,Tumaini lipo
Hebu sikiliza wimbo huu wa Martha Mwaipaja
umenigusa mpendwa. ubarikiwe sana kwa ujumbe huu wakuturudishia tumaini kwamba Mungu bado yuko katika kiti chake cha enzi. Najua Mungu hajatuacha japo mwanadamu wakati mwingine huangalia mazingira yake na kutoa hitimisho lakukatisha tamaa lakini najua bado Mungu yu pamoja nasi. isaya 43:1-2, 8-9,
ReplyDeleteTumaini bado lipo,Tumaini bado liipo tumaini tumaini bado liipo tumaini bado liipo,huu wimbo kwakweli unanitiaga nguvu sana yakuendelea mbele,Ujumbe unatia nguvu tunamshukuru Roho Mtakatifu kwa kutumia watumishi wake
ReplyDeleteBARIKIWA,UJUMBE MZURI SANAA
ReplyDelete