Jenga
Madhabahu Ya Mungu Aliye Hai
*Kutoka 8:22-23
“ Nami siku hiyo nitatenga
nchi ya Gosheni watu wangu wanayokaa ili hao mainzi wasiwe huko, ili kwamba
upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi Bwana kati ya dunia name nitatia mpaka kati
ya watu wangu na watu wako, ishara hiyo
italetwa kesho.”
-Nitatenga nchi, Nitaweka
mipaka. Wakati misri wanapitia mapigo mazito Bwana aliweka mipaka kati ya eneo la Gosheni
walikokaa Israel, eneo hilo likatengwa
likawa na ulinzi wa Mungu.
-Unaposimama juu ya
madhabahu ya Mungu aliye hai ndani ya nchi, Bwana anasema walikuwepo watu
wanaomba na kumtumikia katika hali ya unyenyekevu, Bwana atashuka mahali hapa
tuombapo na kuitenga nchi yetu na maangamizi.Tunapojenga madhabahu ya Mungu aliyehai ndani ya nchi ,
tunasimama mahali hapa na kuomba Mungu aliye hai, anashuka na kuponya nchi
yetu.
*2Mambo ya nyakati 7:15
“Sasa macho yangu
yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.”
*2Mambo ya Nyakati 7:13-14
“Nikizifunga mbingu isiwe
mvua, tena nikiamuru nzinge kula nchi au nikiwapelekea watu wangu tauni, ikiwa
watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba na kutafuta uso , na kuziacha njia
zao mbaya, basi nitasikia toka
mbinguni na kuwasamehe dhambi yao
na kuiponya nchi yao”.
-Lazima nchi yetu iponywe na magonjwa , lazima tuombe nchi yetu
iponywe na umasikini, lazima tuombe Mungu nchi yetu iponywe na magonjwa
mazito.Tuombe Mungu alete uzima na uhai juu ya nchi yetu, Tanzania yetu lazima iwe
na uzima, lazima tuombe na kuamuru ustawi na kukua kwa uchumi wetu, hii ndiyo
madhabahu ya Mungu aliye hai. Bwana aweke mipaka sasa kati ya Ukimwi na
watanzania, tuombe Bwana Mungu aweke mipaka kati ya umaskini na maisha
yetu.Madhabahuni pa Bwana huleta mageuzi
kwa wote wanaokimbilia pale.
-Hakikisha familia yako,
mali zako, wewe mwenyewe na watoto wako mnakuwa mmeungamanishwa katika
madhabahu ya Mungu aliye hai kupitia damu ya ukombozi ya mwana kondoo wa Mungu
YESU KRISTO MKOMBOZI.
-Bwana anakwenda kufanya mageuzi
katika nchi yetu , mageuzi ya kiroho na kiuchumi.
*Ayubu 42:10
“Bwana akaugeuza uteka wa Ayubu”
-Bwana ninaomba kikamilifu kwa moyo wa dhati, ushuke
na kufanya mageuzi katika nchi. Leo sasa tunapoomba mbele ya Mungu mwenye
nguvu, tuombe Bwana afanye mageuzi , badala ya vita atupe amani, badala ya
magonjwa atupe afya njema, badala ya umaskini atupe heshima, badala ya vifungo
atupe uhuru, badala ya laana atupe Baraka.
*Yeremia 31:13-14
“Maana nitageuza
masikitiko yao kuwa furaha, nami
nitawafariji na kuwafurahisha waache
huzuni zao, name nitaishibisha roho ya makuhani kwa unono na watu wangu
watashiba kwa wema wangu, asema Bwana.”
No comments:
Post a Comment