Haya wapendwa wangu,poleni kwanza maana wiki ijayo
sikutokea nilikuwa busy kidogo na huduma,yote ni katika kuujenga mwili wa
Kristo
Leo tunaendelea na vitu muhimu vya kuangalia kwa mtu anayetarajia kuwa
mwenzi wako. Tulianza na jambo muhimu juu ya Uhusiano wake na Mungu tukachambua
vipengele mbalimbali katika hapo inawezekana kabisa sijamaliza vyotee maana
eneo la uhusiano wa mtu na Mungu ni pana sana,ila kwa kifupi yale ni mambo
muhimu ya kuzingatia.
Tuendelee...
1.
Historia yake ya nyuma ikoje
Huyu mwenza ni vizuri ukajua historia yake ya nyuma kama
utakuwa na neema akuambie yeye mwenyewe au ujiweke kuwa mchunguzi wa
kujitegemea katika hilo maana si ni jambo la maisha yako,kwahiyo lazima
uhakikishe linakupa amani.
Nimeona vilio katika ndoa watu wanakuja kujua kwamba
wenzi wao walikuwa hivi na vile wakati tayari wameshaingia,mtu anaona kama vile
mwenzake amemchezea picha yaani filamu kabisa,kwasababu niambie mwenzangu
umeshaingia ndio unajua hee mpendwa huyu kumbe ana watoto,au alikuwaga
mwizi,jambazi,mahusiano e.t.c. Kwakweli inauma sana kujua jambo hilo kwa
kuchelewa au ukiwa tayari kwenye ndoa.
Ni vizuri mtu ujue mapema halafu ujievaluate kama unaweza
kuyabeba mambo hayo,ujipime mapema kabisa hivi kweli mimi jamani nitaweza
kuolewa au kumuoa mtu mwenye historia ya namna hii,je nitaweza kulelea mtoto wa
mtu mwingine? Je nitaweza kuibeba aibu hii ya mwenzi wangu au nitajisikia hata
vibaya kutembea nae maana yeye alikuwa na historia hii.
Ukiona huwezi usijitese na pia sio vizuri uingie na
ukaanze kumtesa mwenzako na maneno ya manyanyaso ooh ndio maana ulikuwa
a,b,c...z, mpendwa kuwa muwazi mapema
Ili kuwa na amani na kutoingia katika mahusiano halafu
yavunjike kwa ajili ya mambo ya historia zingatia haya;
a. Uliza
historia mapema
Ni vizuri
katika hatua ya mwanzo kabisa ya urafiki kabla hamjafika kutambulishana kwa
wazazi,ndugu na jamaa kujua kwa uwazi kabisa historia ya huyo anayetaka kuwa
mwenzi wako. Hii itakusaidia kuamua kuendelea au kuachana na mahusiano hayo
mapema. Itakupunguzia kama sio kukuepushia kabisa na machungu ambayo
yangejitokeza huko mbeleni
b. Kupata
muda wa kutosha kuijua na kutathimini hiyo historia
Jipe muda
usikimbie sana,usifanya fasta fasta,utakua mtu anakuja kwa spidi kali sana
anataka aoe kumbe kuna kitu ameficha kikubwa anataka fasta usipate hata muda wa
kukihisi hicho kitu kuwa makini mpendwa.
Na ujue kabisa
kwa akili zako hutaweza ila Mungu atakuwezesha,na atakuwezesha tu utakapokuwa
na mahusiano mazuri na yeye,Amen! Hebu tusome pamoja huu msitari kutoka katika
Yeremia 33:3 “ Niite nami nitakuitikia
nami nitakuonyesha mambo makubwa usiyoyajua” ukiangalia huu mstari utaona
jinsi Mungu anavyosema kwamba muite na yeye atakuitikia na kisha atakuonyesha
mambo makubwa usiyoyajua. Kwa hiyo hata kama kuna vitu anaficha hataki uvijue
ukimwita Yesu atakuonyesha mpendwa wala usiwe na wasiwasi. Mungu ni mwaminifu
sana sana yaani ninayo kila sababu ya kusema hivyo maana nimeuona uaminifu wake
katika mambo mbalimbali kwangu na watu wengine walioamua kumtegemea.
Mungu anaweza
mpendwa mtegemee tu yeye peke yake na uweza wake.
2.
Angalia jinsi anavyoishi na watu
Ukitaka kujua tabia halisi ya mtu angalia jinsi
anavyoishi au kutenda kwa watu ambao hawajui au watu wa hali ya chini. Kama
mmekwenda mahali kunywa juice angalia jinsi anavyomwambia au kumkosoa yule
muhudumu kama amesahau kitu, je anamuambia kwa kumwelimisha kwamba amekosea? Au
anamwambia kwa dharau na kumkashifu? Hapo utajua kabisa huyu mtu mmh nikija
kukosa nitakoma.
Je kama ni mtu ambaye ana uwezo wa kifedha au amesoma
kiasi ,akikutana na watu ambao hawana uwezo au ambao hawajasoma kama yeye
anaongeaje nao,anawajali,anawaelimisha? au ndio anawaonyesha dharau kubwa
kwasababu yuko katika kiwango cha tofauti na wao.
Neno la Mungu katika Mithali 17: 5 linasema “Amdhihakiye maskini humsuta Muumba wake; Naye
aufurahiaye msiba hatakosa adhabu”.
Mtu anayemdharau masikini au mtu mwenye shida ni chukizo
mbele za Mungu na ataadhibiwa. Kuwa makini na mtu wa jinsi hii maana atakuja
kukuletea matatizo baadae. Ila pamoja na yote hata kama ana hiyo tabia unaweza
pia kumshauri kama ni mtu ambaye anapenda kubadilika ataiacha ila kama ni mtu
anayejihesabia haki hataiacha hapo ndio inabidi uchukue hatua uamue kama
unaendelea na huo uhusiano au lah.
No comments:
Post a Comment