Samwel Mwangu mwimbaji wa nyimbo za Injili |
Blogger: Naomba majina yako kamili,na je unatumia Jina tofauti la kisanii?
Tungependa kulijua pia ili jamii iweze kukutambua kwa urahisi.
Mwambaji: Samuel Mwangu
Blogger:Umeokoka na unaabudu
wapi
Mwimbaji: Nimeokoka na
ninaabudu katika kanisa la TAG, CITY HARVEST, Dar es salaam.
Blogger Historia yako kwa Kifupi ya kuimba,yaani ulianzaje na wapi?
Mwimbaji: Nimezaliwa 1988,
katika familia ya kikristo, huduma ya uimbaji nimeanza mwaka 2003 katika kwaya,
kanisa la Mission to Unreached church (MUAC), mkoani pwani, mlandizi. Mwaka
2010 Mungu aliniwezesha kuanza kujitegemea katika uimbaji, mpka hivi sasa kwa
neema ya Mungu naendelea kutumika.
Blogger:Katika kuimba kwako je umeshatoa Album au
single yoyote? Itaje ina nyimbo ngapi?
Mwimbaji: Mpaka hivi sasa nina albam mbili, ya kwanza inaitwa NINAISHI
SABABU YA MUNGU nay a pili inaitwa NJOO VILE ULIVYO ( UTAN’GAA KAMA JUA.)
Blogger: Wimbo unaoupenda katika nyimbo zako
Mwimbaji: NJOO VILE ULIVYO
ninaupenda zaidi.
Blogger:Ni kwanini unaupenda huo wimbo/nyimbo
Mwimbaji: Kwa sababu unaelezea
zaidi juu ya pendo la yesu katika maisha yetu wanadamu, pia biti ya wimbo huu
na mpangilio wa maneno yake ni nzuri mno.
Blogger:Nani anasambaza kazi zako? Je anakusaidia
vizuri?
Mwimbaji: Kwa sasa
nasambaza mwenyewe, bado sijafanikiwa kupata msambazaji.
Samwel Mwangu akiwa katika utumishi wa Kumuimbia Mungu |
Blogger:Kuna mafanikio gani umeyapata katika
kuimba kwako nyimbo za Injili
Mwimbaji: Mafanikio
sio makubwa kwa sasa, kwani bado sijapata soko la kuuza kazi yangu, na pi bado
sijafanya promo ya kutosha.
Blogger:Umekutana na changamoto gani katika
safari yako ya kuimba
Mwimbaji: Changamoto
kubwa ni swala la fedha, imekuwa ni kikwazo kikubwa kwangu. Na pia kupata
msambazaji.
Blogger:Unaonaje Music wa Injili hapa Tanzania?
Mwimbaji: Music wa injili
Tanzania unakuwa kwa kasi kubwa sana, ila soko bado lipo chini, wizi wa kazi za
wasanii umekuwa mkubwa sana, watu wanachukulia kawaida.
Blogger:Na Unatoa Ujumbe gani kwa waimbaji wa
Nyimbo za Injili ambao kwa njia moja au nyingine wanajisahau na kujichanganya
na mambo ya dunia hii
Mwimbaji: Wito wangu kwa
waimbaji ni kutunza maisha yao, wajali utakatifu wasiondoe uthamani wao kwa
sababu ya changamoto wanazopitia, iwe ni
binti ua kijana wa kiume.waishi maisha ya mfano, ili Mungu ajitukuze katika
maisha yao.
Blogger:Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unachofanya
Mwimbaji: Ni mwandishi wa
habari
Blogger:Je kimaisha je uko wapi? Umeoa au Hujaoa
bado? Watoto wangapi?
Mwimbaji:Bado sijaoa, ninaishi mwenyewe hapa
Dar es salaam.
Hata Kinanda anapiga |
Blogger:Una Ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa Tanzania
Mwimbaji: Wasikate tama katka
kutumika, wamtangulize MUNGU mbele zaidi kuliko PESA.
Blogger: Una Ujumbe gani kwa Jamii inayoburidishwa na nyimbo za Injili
Mwimbaji: Waendelee
kutusupport kwa kununua kazi zetu.
Blogger:Asante sana kwa
Muda wako,Mungu akubariki na kukuinua unavyoendelea kumtumikia kwa
uaminifu.Amen
Mwimbaji :Asante sana kwa ushirikiano wako.
Amina Ubarikiwe Samwel, ukitaka kumkaribisha kwa huduma yuko tayari kabisa tuwasiliane, Haleluya
No comments:
Post a Comment