Habari
mpendwa wangu, Karibu tena wiki hii nyingine nzuri Mungu ametupa tuzungumze na
kushauriana
Leo
tunaendelea na somo letu zuri tuliloanza wiki iliyopita la Usioe au Usiolewe
kwa Msukumo wa Sababu hizi Kumi zisizofaa
Halleluya
nasikia furaha sana kupata kibali cha kuzungumza na wewe siku ya leo.
Haya
tuendelee na zile sababu tano zingine;
6. Hofu ya kujitegemea
Kuna
watu wengine ni tegemezi sana kwa wazazi wao,utegemezi huu unaweza ukawa
umesababishwa na malezi wazazi waliwalea au yeye mwenyewe tu ni mvivu.
Utakuta
mzazi anamfanyia mtoto kila kitu, atamtafutia chuo, atampeleka chuo,
atamtafutia kazi, atamtafutia kiwanja,kupikiwa, kufuliwa etc,yaani mtoto
anafanyiwa kila kitu kiasi kwamba yeye mwenyewe hana nafasi ya kuwaza na
kufanya vitu peke yake. Sasa hapo pia inategemea na mtoto mwenyewe kama
anapenda hiyo hali ndio atabweteka hivyohivyo.
Sasa
basi akiona amekaa kwao na umri unaenda sana na wazazi labda wanamshauri apange
nyumba na kujitegemea yeye anapata woga kwasababu alizoea kufanyiwa kila kitu
ili kukwepa hayo anaamua aolewe au aoe na yeyote anayejitokeza ili tu apate pa
kutegemea.
Sasa
ndugu yangu kama umemuoa mtu au umeolewa na mtu kwasababu ya huo woga unafikiri
kweli utaiweza ndoa, na je huyo uliyemtegemea akashindwa kufikia hayo matarajio
yako ya utegemezi si utakimbia, nakuomba leo badili mtazamo usichukua uamuzi wa
kuingia kwenye ndoa kama sehemu ya kumtegemea mwenzio akufanyie fanyie,
badilika leo ndugu yangu, kuolewa ni kuzuri pale tu panapofanyika vile Mungu
anataka na kama nilivyosema mwanzo kuna sababu nzuri tu za kuoa au kuolewa
lakini sio hofu ya kujitegemea.
7. Hofu ya kumuumiza
mwenzako
Inawezekana
ulikuwa kwenye mahusiano ya uchumba, lakini muda ulivyoendelea ukaona kwamba
huwezi tena kuendelea na huo uhusiano inawezekana kwa sababu nzuri tu
Sasa
labda ukiangalia muda ambao mlikaa katika huo uhusiano, mambo mliyoahidiana na
kufanya pamoja, labda jinsi jamii inavyowatambua, ukaingiwa na hofu kwamba
kwakweli sitaweza kumwambia huyu kaka au dada kwamba siwezi kumuoa au kuolewa
naye kwasababu nitamuumiza sana. Matokeo yake unamuoa au unaolewa na mtu ambaye
kiukweli hukupenda ila ni kwasababu uliogopa kumuumiza.
Sasa
vile vitu vilivyokusababisha utake kufanya uamuzi wa kuachana nae na wewe
ukashindwa kwasababu uliogopa kumuumiza, ujue kwenye Ndoa ndio utaviona vizuri
sana tena clear, sasa sijui utamlaumu nani unaanza kukosa raha na mwisho kama
hutakuwa makini na Mungu kuingilia kati hiyo ndoa inaweza kuvunjika kabisaa.
Au
mwingine anaamua kabisa kumwambia mwenzake kwamba kutokana na jinsi huu uhusiano
unavyoenda naona tuvunje kabla hatujaenda kupata matatizo katika ndoa, sasa
mwingine hasa wakina dada Analia hapo mawiki na mawiki, na mwingine anatishia
kujiua, sasa mkaka akiona hivyo anaogopa kwamba mwenzake atapoteza maisha
kwasababu yake kwahiyo analazimika kuendelea na mahusiano hadi ndoa.
Je
unategemea akimuoa huyo aliyetishia kujiua na bado ulikuwa na sababu za msingi
za kuvunja uhusiano unafikiri maisha ya ndoa yatakuwaje? Hebu tafakari
Nakumbuka
kuna kijana aliniambiaga namuoa fulani kwasababu unajua nimekaa nae miaka mingi
sasa nimempotezea muda japo simpendi lakini namuonea Huruma,hiyo si sawa bora
uchumba uvunjike kwa machozi kuliko Ndoa jamani naomba kusisitiza, Haleluya
bado unanipenda jamani maana kuna watu wanapenda kung`ang`ania wee kama
kakukataa jamani sio mwisho wa Safari na wala hutakufa kwa kumkosa tena baadae
ukijam kutafakari kwanini nilikuwa
napoteza muda kwa mtu kama huyu utajicheka sanaaaaa cause they don’t deserve
you, Wewe ni mtoto wa Mfalme Bwana, Ambassador of Christ why worries enhee!
Aminaaaa!
8. Kuwa mshauri wa Mtu
Yamkini
kuna mkaka au mdada akakushirikisha machungu anayopitia katika mambo ya
mahusiano, tena nimegundua ni strategy watu wanatumia siku hizi anakwenda
kumweleza mtu mambo anapitia katika mahusiano anajiliza weee huko kumbe anataka
awe na mahusiano naye. Jamani tuwe makini shetani kila siku naye anatunga mbinu
mpya kama Teknologia inavyobadilika nay eye anabadili mbinu hivyohivyo.
Sasa
wewe mkaka mdada kaja na kilio kwamba amepata mateso katika mahusiano yake ya
huko nyuma, labda alibakwa, au alifanyiwa unyama mbalimbali, kwakweli hivyo
vitu vikakuumiza ukaona mmh huyu kwasababu amenishirikisha acha tu nimuoe ili
niwe namsaidia kumshauri, Kuwa makini kama hiyo tu ndio inakusukuma kumuoa ujue
maisha ya Ndoa ni ya milele kifo tu ndio kitawatenganisha sasa kama utakuwa
uliamua juu juu itakugharimu sana ndugu yangu.
Wewe
kama ni mshauri fanya kazi yako ya ushauri na muombee lakini uwe makini na
maamuzi yanahusu mahusiano na huyo mpenda, uwe na uhakika kwamba ni mpango wa
Mungu na sio msisimko wako au Huruma yako inakufanya umuoea, Halleluyaaaa
9. Kufanya Tendo la
Ndoa kabla ya Ndoa
Inawezekana
mmekuwa kwenye uchumba mkaanguka na kufanya tendo la Ndoa,
Tendo
la Ndoa ni kwa ajili ya Ndoa tu na si vinginevyo, ndivyo Mungu aliweka. Sasa
basi kama mtu amejikuta kaanguka basi ATUBU haraka sana na kuacha. Halleluya,
na Ujue Mungu ni mwaminifu atakusamehe. Hapo utakuwa na kazi pia ya kujisamehe
mwenyewe ama sivyo hiyo hali itakusumbua sana katika Ndoa.
Kama
wachumba au watu wako katika mahusiano wakaanguka na kufanya tendo la Ndoa na
baadae mmoja akaona kwamba kuna tabia au vitu vitamfanya avunje mahusiano, Hapo
ndio inakuwaga shughuli sana hasa kwa wadada wengine utakuta wanang`ang`ania
lazima unioe kwasababu umeniharibia usichana wangu kwahiyo mkaka atakuwa tu
kalazimishwa kuoa huyo dada labda kwa Huruma na vitisho lakini zile tabia
alizokuwa nazo mwanzoni kumbuka kwamba hazitabadilika tu kwa sababu tu amekuoa
au umemuoa zitakuwa palepale. Hiki kinaweza kusababisha matatizo makubwa katika
Ndoa na hadi kusababisha kuvunjika, kwahiyo mpendwa unavyomng`ang`ania huyo
kaka au dada kuwa makini sana ni NINI MSUKUMO wako ? Mungu anasemaje katika
Hilo? Unajua kama ni aibu Mungu amesemaje jamani Tumpe yeye aibu zetu zoote sio
moja nay eye atatusitiri na ndio maana yeye ni Mungu Mkuu. Sasa kung`ang`aniza
ndoa ili ufiche aibu mmh si sawa…Helooo
10. Kupata Ujauzito
Haya
mdada umekuwa na mahusiano huko na mtu ambaye labda kila siku anakupa presha,
leo yuko na Jane, kesho yuko na Pendo, leo Lilian ,kesho Clara then jana Manka,
wewe sasa kwasababu unajua kupenda mpaka hujitazami mwenyewe unang`ang`ania na
sasa kwasababu ameshajua wewe ndio umefika atakuambia chochote na hadi
atakushawishi mfanye tendo la ndoa kabla ya ndoa na wewe ukakubali, halafu
baadae ukapata ujauzito, sasa wewe kwasababu ya ule ujauzito na unajua wazazi
wako walivyo wa Kiroho na hawapendi hiyo mambo umefanya unamng`ang`aniza huyo
jamaa akuoe tena kwa vitisho nitakunywa sumu, ooh nitakulaani nakadhalika
nakadhalika, sasa wewe unafikiri akishakuoa ndio atabadilika na ile style yake
ya kuchange wadada ujue ataendelea hivyohivyo sasa unaaza kujuta, na usipokuwa
makini ndoa itakuwa Ngumu kama sio kuvunjika kabisa.
Kwakweli
single parenting inauma lakini ni bora tu Utubu kwa Mungu wako ulee mtoto wako,
Mungu ni mwaminifu nimeona wadada wenye watoto wawili wakiolewa ndoa tena ya
Heshima, kwahiyo usishushe viwango vya Mungu, mjue kwanza Mungu na umwamini
kwamba anakuwazia mema , usitengeneza Muujiza , acha mtenda miujiza akutendee
na hapa hutaishi maisha ya majuto.
Haleluya
asante sana kwa kuwa pamoja nasi leo,nafikiri Roho Mtakatifu ataendelea
kukufundisha Zaidi hili somo na utalielewa, Kitu kikubwa nataka nikuombe
usikate Tamaa Mungu wetu ni wa Majira na Nyakati, Ujue wakati wako unakuja
tutakula tu Plau na kuvaa Sare haleluyaa, Tembea kwa Ushindi, Usiwe na
Hofu,UTAOLEWA NA KUOA TU kama ndio desire yako, maana yeye ndio anatupa Desires
of our heart, Aminaaa
Tuonane
Tena wiki Ijayo mambo mazuri yanakuja, Haleluyaaa
MBARIKIWE,
Endelea
kutembelea Rejoice and Rejoice Blog mengi na mengi sana yanakuja, Mungu
anafanya mambo makubwa sana!
No comments:
Post a Comment