Mpendwa
wangu Shalom,
Karibu
tena katika Makala haya ya Uchumba hadi Ndoa, yanayoletwa kwenu na Washauri
Wenu wa Ndoa na Mahusiano.
Wiki
mbili zilizopita tuliangalia sababu 10 zisizofaa kuamua kuoa au kuolewa, ambapo
tulipata nafasi ya kuchambua mambo mengi na ya muhimu.
Basi
leo Karibu tena tuendelee na Somo lingine, Leo tutazungumzia Sababu Kumi(10)
zinazofaa kumfanya mtu aamue Kuoa au Kuolewa;
1. Ndoa ni Mpango wa
Mungu
Mungu
ndiye Mwanzilishi wa Ndoa, tunasoma katika Mwanzo 2: 18 “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia
msaidizi wa kufanana naye.”
Mungu
aliona si vema mtu awe peke yake na ndipo akamfanyia msaidizi(MKE) wa kufanana
naye. Kwahiyo unaona kabisa Ndoa ilikuwa ni mpango wa Mungu na sio kwamba baba
yetu Adamu alijiamulia tu kwa msukumo wake mwenyewe. Na hii muhimu sana kwa
Wakristo kujua kwamba Mungu anatuwazia mawazo mema, yeye bila kuombwa na Adamu
anaona huyu ngoja nimpatie mwezi wake ambaye anafanana naye, Mungu alijua
akimpa ambaye hawafanani itakuwa kasheshe. Mungu ni Mpangaji Mzuri sana
kwakweli Uzuri wake haulezeki nikiangalia jinsi amefanya mambo yake huwa
namshangaa na kumsifu tu.
Katika
maisha yako ya kila siku najua umekuwa na mahitaji mbalimbali ambayo
unayapeleka mbele za Mungu kwa njia ya maombi, kwa mfano Kufaulu mitihani,
kupata kazi, kupona magonjwa , kupata kazi nakadhalika nakadhalika, Sasa kama
umemuomba Mungu akakujibu juu ya hivyo vitu vingine kwanini kwenye swala la
Ndoa usimwamini Mungu hivyohivyo.
Kabla
ya kupata mwezi na baada ni vizuri kuwa katika hali ya maombi ili mapenzi ya
Mungu yatimizwe, ili Mungu akupe mtu yule aliyemkusudia ambaye unafanana naye.
Kwasababu ukipata unayefanana nae mtaishi kwa upendo na kuchukuliana.
Kwahiyo
ni ombi langu kwako ndugu yangu mpendwa kwamba Mungu akupe neema ya kukaa
katika maombi katika hatua yoyoye ambayo uko, iwe hujapata mwenza , au
umeshampata au uko ndani ya Ndoa.
Hiyo
itakusaidia sana kuwa na maisha ambayo Mungu amekukusudia kwasababu utakuwa
unatembea katika mpango wa Mungu
2. Kuonyesha Upendo wa
Mungu kwa Mwenzi wako
Mungu
wetu ni Upendo na upendo wake ni wa Agape, yeye alitupenda wakati sisi tuko
katika dhambi na wala hatuna chochote ambacho tumempa.
Upendo
wa Mungu sio kama ambao baadhi ya watu wanao, hauna masharti, watu wengi wana
upendo wa masharti ule wa Nipe Nikupe, nakupenda kwasababu ya Pesa, au
nakupenda kwasababu ya najua nitapata upendeleo fulani fulani, na siku hizi
imekuwa hatari sana vijana wengi wanaoa au kuolewa na watu kwasababu hao watu
wana vitu fulani kama magari, nyumba, hela, au vyeo
Lakini
Upendo wa Kweli ni ule wa Mungu ambao hauna masharti, tunapaswa kuingia katika
Ndoa ikiwa ni njia nzuri ya kuonyesha Upendo wa Mungu kwa wenzi wetu.
Ndoa
ni sehemu sahihi kabisa ya wenzi kuonyesha upendo wa Agape kwa kila
mmoja,kumpenda mwenzako akiwa mzima au mgonjwa, akiwa na fedha ua hana, akiwa
na cheo au asipokuwa nacho, kumuonyesha mwenzako upendo bila kusubiri kupata
chochote kama Mungu na Kristo walivyotupenda kwanza.
3. Kuonyesha Upendo wa
Kweli kwa Mwezi wako
Ndoa
ni sehemu muhimu sana ya kuonyesha upendo kwa mwezi wako, kwahiyo ni vizuri
kuoa au kuolewa kwa makusudi ya kutaka
kuonyesha upendo kwa mwenzi wako
Katika
Ndoa kunatakiwa kuonyesha aina tatu za Upendo;
·
Phileo ambao ni ule
upendo wa Kimahaba kwa mpenzi wako, kwahiyo unapooa au kuolewa ndugu mpendwa
ujue una jukumu la kuonyesha upendo wa kimahaba kwa mwenzi wako
·
Eros ni vizuri kuingia
kwenye ndoa kwa shauku ya kutaka kuonyesha upendo wa kimapenzi kwa mwenzako,
kuwa Tayari na furaha kwa ajili ya ile zawadi kubwa ya Tendo la Ndoa Mungu
aliyoiandaa
·
Agape wanandoa pia wana
jukumu la kuonyesha upendo wa Mungu kwa kila mmoja kama nilivyokwisha kuelezea
hapo juu
Kwa hiyo Upendo kwa mwenzi wako
ni jambo la msingi sana nan i msukumo unaoruhusiwa kufanya maamuzi ya kuingia
katika Ndoa, kwahiyo mpendwa kama hujaingia hebu jichunguze je kuna upendo , ni
nini
Msukumo wako?
4. Shauku ya kuazisha
familia pamoja
Mungu
ametupa Ndoa ni Zawadi kubwa sana ya kuanza familia pamoja, na familia sio
lazima watoto maana mnaweza msijaliwe watoto, kuna familia nyingi tu hawajapata
watoto na wanaishi kwa furaha
Watu
wowote ambao Mungu atakupa uishi nao basi ndio familia yako, kwahiyo katika
hali yoyote ambayo utajikuta uwe na watoto au usiwe nayo machoni mwa Mungu wote
mna thamani, na usiingie kwenye ndoa kwa msukumo wa Mtoto mtoto tuu, kwasababu
asipokuja au akichelewa utapata msongo wa mawazo na itakuwa ni mwanzo wa
shetani kukuibia furaha ya Bwana ndani ya Ndoa yenu.Halleluya wapendwa
5. Shauku ya kuwa na
mwenzi utakayeshirikiana naye tendo la Ndoa kama Mungu anavyotaka
Haleluya
pia kuingia kwenye ndoa kwa matarajio ya kuwa kushiriki tendo la Ndoa na mwenzi
wako ni jambo zuri lakini Isiwe ndo
msukumo pekee tu wa kuingia kwenye ndoa kama nilivyozungumza katika sababu
kumi zisizofaa za kukufanya uingie katika ndoa.
Kama
utaamua kuingia kwenye Ndoa kwa msukumo huo wa tendo la Ndoa tu , sasa mwenzako
akapata matatizo ya kiafya ambayo hayatamruhusu kufanya hilo tendo, unafikiri
itakuwaje si matatizo?
Hili
tendo pia ni zawadi Mungu ametoa kwa wanandoa tu, kwahiyo ewe kijana mwenzangu
muombe Mungu akuwezeshe ujizuie hadi utakapoingia kwenye ndoa, utakuwa huru Zaidi.
Naomba
nisisitize jambo hapa, yamkini umeokoka ukiwa huko nyuma ulishafanyaga hilo
tendo au ulianguka ukafanya hilo tendo, Nakusihi TUBU, na adhimia moyoni mwako kwamba unakwenda kutembea katika
usafi na uweke mwili wako kuwa dhabihu mbele za Mungu kwamba Hutafanya hadi katika
Ndoa, nakwambia mpendwa Mungu ni mwaminifu tena atakuheshimu na atakuvusha na
Shetani atashindwa, Halleluya, ujitambue kabisa kwamba wewe ni Kuimbe Kipya na
mwili wako ni Hekalu la Roho Mtakatifu usikubali watu wakuchezee chezee,
Aminaaaa.
Hata
akaja mkaka anatoa mapepo 100 kwa dakika 5 usidanyanyike yeye ni mwanadamu tuu,
simama Imara na Mungu ndio ataona moyo wako na kukuletea yule aliyemkusudia
katika maisha yako, na hayo yatakufanya uwe na Ndoa yenye Ushuhuda kwasababu
ulimuheshimu Mungu, Haleluyaaaaaa….
Wapendwa
wangu Mungu awabariki naomba tukutane tena wiki ijayo tukiendelea na sababu
tano zilizobaki, Mungu aendelee kujifunua kwamba wewe unayemngoja tena mngoje kwa
furaha maana Bwana anakwenda kukutokea na utamshangaa, wewe ambaye umeshapata
endelea kuomba ili iwe kweli ni mapenzi yake na wewe uliekwisha kuingia endelea
kumtafuta Bwana akupe hekima ya kuishi na mwenzi wako, na Baraka za Baba yetu
Ibrahimu ziambatane nanyi wote, Amen!
Endelea
kutembelea Rejoice and Rejoice Blog mambo mazuri yanakuja,
Halleluyaaaaaaaaaaaaa
Very nice..a great article! Stay a blessing!
ReplyDelete