Karibu
tena katika Makala haya ya Mahusiano na Ndoa, leo Washauri wenu tuko Tayari
kabisa kuwaletea somo zuri kabisa la kujiepusha kuingia katika ndoa kwasababu
tu ya misukumo isiyofaa
Leo
tutaanza kuongea juu ya kuolewa au kuoa kwa msukumo wa sababu tano zisizofaa,
sababu tano zingine tutamalizia wiki ijayo, Karibu Sana
Tunaposema
sababu zisizofaa ina maana kuna sababu Nzuri tu zinazofaa za kwa mtu kuamua
kuoa au kuolewa sasa hizo tutaleta baada ya kumaliza hili
1. Kuwa huru na ulinzi
au kufuatiliwa na Wazazi
Vijana
wengi wameamua kuoa au kuolewa kwasababu labda wazazi wao wamekuwa wanaingilia
sana uhuru wao kwa mtazamo wao
Kama
tunavyojua maana pia hata sisi tulikuwa vijana, kijana anakuwa anatamani sana
kuwa huru kujipangia maisha yake labda afanye hivi na vile au arudi nyumbani
usiku au saa ingine asirudi kabisa, sasa mzazi anakuwa mkali atamuuliza maswali
kwanini unafanya hivi, kwanini umechelewa, kwanini unachelewa kazini,
nakadhalika nakadhalika, au labda ana mahusiano mzazi anayatilia mashaka, sasa
kijana mwingine anaona wazazi wanaingilia uhuru wake, Kwahiyo sasa anaamua ili
kuondokana na hiyo adha hawa wazazi wananizingua sana ngoja niolewe tuone
watanifuatilia huko kwa mume au nyumbani kwangu.
Sasa
ni kweli utakuwa umeoa au kuolewa kama huo tu msukumo wa kuoa kwakweli ndugu
yangu sio sahihi, kwasababu baada ya muda maswali na ufuatiliaji ule unaweza
kuanza tena kwa mwezi wako atataka kujua ratiba zako sasa kwasababu wewe ndicho
ulikimbia kwenu huoni kama hapa utakimbia tena, Hebu tafakari kabla hujaamua
hiyo ni sababu kweli ya msingi ya wewe kuolewa…
2. Kukimbia matatizo
ya nyumbani kwenu
Kila
familia ina changamoto zake, wengine uchumi unayumba, nyingine baba mlevi na
mkorofi labda, au magomvi yasiyoisha, wengine kusakamwa, wengine ukaa
uswahilini sana hupapendi kwakweli, sasa kwa kuona hivyo na labda wanakataa
usipange unaamua kuoa au kuolewa ili uwe mbali na kero hizo za nyumbani.
Ina
maana wewe huwezi kuvumilia mawimbi ndugu yangu, kama umeshindwa kuvumilia changamoto
za wazazi wako hivi huyo unayemuona kwamba anakuambia anakupenda sasahivi je
kweli akipata au changamoto utaweza kukaa kweli, maana leo anaweza kukosa kazi,
hela ukajikuta uko katika maisha ambayo hata uliyokimbia kwa wazazi wako ni
mazuri Zaidi, eenhe tuambie utakimbia tena au? Ndio maana leo tuko hapa
kukusaidia na kukushauri lazima utafakari kabla hujaamua ili usije ukaamua
kuingia katika ndoa kwasababu ambazo hata hazina tija, zipo sababu zenye tija
tutakuja kuzifundisha.
Tafakari
ndugu, mdogo na mwanangu, je kuna lingine linalokufanya uamue uchukue huo
uamuzi.
3. Unajiona mnyonge na
hufai wala hustahili na huna sifa sasa akitokea mtu anasema anakupenda unaamua
fasta
Kuna
watu labda mazingira waliokulia au ufahamu walionao juu ya maisha umewafanya wawe
wanyonge na kujiona hawafai, hawastahili, hawana sifa ya kuoa au kuolewa
Inaweza
kuwa labda wazazi waliwalelea katika mazingira ya unyongee sana wakiwaambia
kwamba hawafai, wamekuwa wakijidharau sana, wakijishusha sana
Na
hii hata wanapokuwa na marafiki wanaendeleza hii tabia , kwahiyo hata mashuleni
wanajulikana ni watu wasiofaa, wanyongee sanaa sana, hawana sifa na kibaya wao
wenyewe wanajitambulisha hivyo
Labda
mwingine anavyojiona na umbile lake anaweza kujidharau au kudharauliwa
Sasa
mtu ambaye yuko katika mazingira hayo akatokea tu mtu akawambia anampenda
anaweza kuamua haraka sana kwasababu labda hakuwahi kupata mtu anayemdhamini,
lakini hiyo tu haitoshi kuwa sababu ya kuoa au kuolewa
4. Kumonyesha mtu
aliyekuacha kwamba umeoa au umeolewa
Katika
maisha ya Ujana kuna mambo mengi sana, unaweza ukawa na mtu huyu ukidhani
mnaweza kuja kuoana lakini ikaja ikaishia uhusiano ukavunjika
Mahusiano
yanapovunjika yanaleta maumivu kwa pande zote , sasa mwingine usipokaa sawa
unaweza kwa hasira na kumuonyesha huyo labda aliyekuacha kwamba na mimi naweza
kuoa au kuolewa
Unamuonyesha
kwamba hata wewe bado uko kwenye chati kwamba umepata mtu na huyo mtu tena
anakuoa au anakubali kuolewa , ni kweli inafurahisha na utajisikia vizuri
lakini hii isiwe tu ndio msukumo mkubwa wa wewe kuoa au kuolewa kwasababu
kumbuka unaoa na unaolewa na mwanadamu na yeye atakuwa na madhaifu tu kama
mwanadamu mwingine yeyote wewe olewa au oa tu kwasababu zinazofaa ambazo
tutawaletea wiki zijazo tukimaliza hili. Usifunge ndoa kwa kujionyesha kwamba
wewe ni kiboko, uko juu na hushindwi, au kwasababu unataka kumkomesha mtu.
5. Kwasababu marafiki
zako wameolewa
Yamkini
ulikuwa na marafiki zako mmemaliza wote chuo au mnafanya nao kazi au biashara
au mko nao kanisani mko rika sawa, sasa wanaoa na kuolewa na unajikuta umebaki
peke yako, unaanza kupata msongo wa mawazo jamani mimi nimemkosea nini Mungu,
mbona hakuna anayenikubali mimi au anayeniona mimi. Je wakati wa Bwana umefika
mpendwa. Mimi kuna jambo Mungu alinifundisha ikifika majira na wakati wake
kwakweli lazima litimie. Katika Mhubiri 3: 1 neno la Mungu linasema “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati
kwa kila kusudi chini ya mbingu.” Mpendwa wangu usifunge ndoa na mtu tu yeyote
kwasababu tu unakimbizana na mikumbo, hapana kwasababu unaweza kujikuta unakaa
katika hiyo ndoa uliyoingia kwa mwezi mmoja tu kwasababu haikuwa wakati wake,
ulifanya kwasababu wenzako wamefanya. Zipo sababu nzuri tu za kuoa na kuolewa
lakini sio hii mpendwa.
Kabla
hujaamua kukubali kuolewa jiulize tu ukiwa peke yako na Mungu atakusaidia hivi
kweli huu msukumo unaonisukuma nioe ni kweli ndio tu sababu ya kufanya haya
maamuzi.
Ni
muhimu kutafakari kwasababu Ndoa ni maisha, kama Mungu amekupa miaka mingine
hamsini hapa duniani kumbuka utakuwa unaishi na huyo mtu je uko Tayari?
Halleluya
mpendwa wangu, Tuonane tena wiki ijayo tukiendelea na zile sababu zizofaa
zilizobakia….Barikiwa
Na
ukiwa na kitu chochote usisite kutuandikia nenda kwenye Contacts kuna email na
namba za Simu tutajibu, Aminaa
Aminaa Aminaa, Mkibarikiwa na Sisi tunabarikiwa maana tunafurahi kufanya kile tulichoitiwa
ReplyDelete