Tuesday, June 4, 2013

TAFES Finalist Day: Wahitimu washauriwa kuiangalia dunia kama Kijiji


Baadhi Ya Associates wakifunga kwa Praise

Siku ya Jumamosi ilikuwa ni siku ya pekee kwa wahitimu wa vyuo vikuu pamoja na wanafunzi wengine ambao ni washirika wa TAFES Dar es Salaam.

Mahafali hayo yalihudhuriwa pia na baadhi ya TAFES Associates wa Dar es Salaam ambao baadhi yao walikuwa ndio wasemaji wakubwa.


Mrs Ruth Mlay na Stephen Mkoloma walituongoza kwa Praise ,Tulifunika

Yesu ni Fimbooo Tembeleaaa aah Yesu ni Fimbo...mnaukumbuka

 
Ilikuwa ni siku ya Baraka sana kwa wahitimu maana walipata nafasi kubwa ya kujifunza mambo muhimu yakuwasaidia watakapokuwa wametoka vyuoni.

Associate kama Dr.Sokile, Dr Kimambo, Andrew Kajeguka,Mr Felchism Mramba na wengine waliweza kuelezea uzoefu wao,kile wanachokifanya na kuwapa wahitimu hao ushauri wa jinsi ya kuishi maisha ya ushindi na mafanikio.

Dr Sokile alifundisha juu ya Career Development ambapo Five P na Five E zilielezewa kwa ufasaha,kama hukuwepo kuna kitabu cha Dr Sokile unaweza kukitafuta,pia Robert alivyoelezea juu ya fursa sehemu ambazo hazionekani kama vile katika mashirika ya dini,kufanya kazi na walemavu,kuhudumia jamii ni fursa nzuri sana zinakupatia mwanga wa kutosha,kama tu hutakuwa mtu unayetafuta masilahi tu.


King Chavala aliweza kutuonyesha upande wake mwingine wa kijasiriamali kwa kutoa ushuhuda wa ambavyo ameweza kusimama katika ujasiriamali hata baada ya kupata changamoto ambazo kwa macho ya kibinadamu zinakatisha tamaa.
 
Baadae tulipata lunch nzuri sana,tulifurahi.

Mchana tulikuwa na wakati mzuri sana ambapo Mr Felchism Mramba alifundisha kwa ufasaha juu ya Life After Campus,kwakweli ilikuwa nzuri sana hakuwa anasema tu na wahitimu hata sisi ambao tumemaliza zaidi ya miaka 5 tulijikuta tukifungua macho yetu.

Mr Mramba aliwashauri wahitimu kuingalia dunia kama Kijiji,akiwa na maana kwamba wawe tayari kuwa Global Citizen,hii ina maana kwamba wawe tayari kuingia katika soko la dunia la ajira na Kibiashara,kujifunza Lugha nyingi za Kigeni ili kuweza kuukabili ushindani. Alitoa shuhuda nyingi kwakweli naweza kusema tu kwa neno moja IT WAS SOO INSPIRING na waliokuwepo walibadilishwa fikra zao.
Mr Felchism Mramba akifundisha somo la Life After Campus,kwakweli lilifungua macho yetu wote
Safari ya Associates haikuishia hapo,iliendelea moja kwa moja kwa Brother Semadio kumpa pole kwa matatizo waliyoyapata.
Mwisho ulikuwa hivi na tukasema Ebenezer
 
Tunamshukuru sana Bro Magubu kwa moyo wake alivyoandaa hii shughuli kwakweli ana moyo sana na kazi yake,Mungu akubariki
 
Mungu Ibariki TAFES, Associates na woteee.

3 comments:

 1. І simρlу couldn't go away your website before suggesting that I actually enjoyed the usual info an individual supply to your visitors? Is gonna be again regularly in order to inspect new posts

  My website; Treatments For Hemorrhoids

  ReplyDelete
 2. I every time uѕed to studу article in
  news papers but now as I am a user оf nеt thus from now Ι am using net for poѕts,
  thanks to web.

  Stoρ by my hοmepage Bleeding Hemorrhoids

  ReplyDelete
 3. ilipendeza sana tunamshukuru MUNGU tulipokea na kufurahi.

  ReplyDelete