Pastor Architect Yared Dondo - TAG City Harvest Church |
Upendo wa
Kweli Hungoja – Waebrania. 13:4
Mpango wa Mungu kuhusu
kujamiiana unahusisha mwanaume mmoja na mwanamke mmoja walio ndani ya uhusiano
wa ndoa. Serikali na dunia kwa ujumla hutumia mamilioni ya fedha kwa kinaitwa “ngono
salama”. Hakuna ngono salama zaidi ya iliyo ndani ya mpango wa Mungu!
Tafsiri ya kidunia
kuhusu ngono salama haijaegemea kwenye maadili hata kidogo. Mawazo yao ni kuwa:
“ikiwa hauwezi kuenenda vyema, basi kuwa mwangalifu”.
Tafsiri ya Mungu wa
ngono salama ni kungoja mpaka ndoa.
1 Petro 2:11 “Wapenzi,
nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na
roho”
Maadili ya Kibiblia
huchekwa, hudharauliwa husemwa ni ya kale na yamepitwa na wakati.
Ninashukuru kwa ajili
ya viajana matineja wachache ambao leo wanasema, kuanzia leo na kuendelea,
nitangojea mpaka wakati wa ndoa….. nitaishi sawa na mpango wa Mungu….. na watu
wazima wanaojitoa tena kuwa wasafi na waaminifu. Tumeliruhusu neno
ngono/kujamiiana kuwa neno chafu. Kilichopaswa kuwa taswira njema ya upendo,
ndoa na maskani, kwa sasa kinahusishwa na upotovu/ukimwi/ukahaba/usagaji/ngono
ya jinsia moja.
Jamii inajifunza
kwamba kuna adhabu ya uasherati na uzinzi. Lakini badala ya kurejea kwenye
viwango vya Mungu na kutii sheria za Mungu, jamii husema “wacha tuone
tunachoweza kufanya kukwepa matokeo ya matendo yetu”
Hapa ndipo hatari iko:
ikiwa utaingia kwenye uhusiano wa kimwili kabla ya ndoa:
Hatari 5 za
ngono kabla ya ndoa:
1.
Pendo bandia
Mahusiano yaliyojengwa
juu ya ngono hayadumu! Mkianza na mambo ya kimwili mtajikuta hata hamvutiani.
Hamtakua pamoja kiakili, kihisia au kiroho!
Upo hapo ukiwa hauna
kitu isipokuwa malai/krimu iliyochapika na inazeekana ambayo utaitupa pia!
Lakini…ikiwa kujamiiana kutaanza baada ya ndoa, sehemu nyingine tatu
zitaendelea kukua pia! Hivyo unakuwa na siyo tu mshirika wa kujamiiana, bali
pia rafiki bora zaidi anayekupenda.
Upendo wa kweli
huvumilia, ni halisi na hauna ubinafsi.
Wasichana, pale
mwanaume anaposema “Siwezi kusubiri”, utajua kwamba hakupendi. Pale anaposema
“Ikiwa wanipenda kweli, nithibitishie”, chukulia hilo kuwa tusi na umchape
kibao cha nguvu kiasi cha ubongo wake kupiga kelele kama kengele za kanisa
wakati wa asubuhi yenye baridi!
Hatari za upendo wa
bandia..
2.
Madhara kihisia
Mabinti wadogo:
Tafiti zinaonyesha
uhusiano wa moja kwa moja baina ya ngono kabla ya ndoa na matatizo binafsi ya
kihisia… Kujihisi mkosaji/wasiwasi/kupoteza kujiheshimu
Kujihisi una hatia
ndiyo hisia inayoweza kutuharibu zaidi.
Hukukosesha usingizi,
amani, furaha, kujithamini na uhusiano wako na Mungu.
Hukuacha umevunjika
vunjika, ukiwa hauna uhakika na kutoweza kuzalisha matunda.
Na kisha hupoteza ule
“mng’ao” unaoambatana na usafi.
Sikieni haya mabinti,
na nitawaambia namna wanaume hufikiri…
…..kuna fumbo fulani
kuhusu yasiyojulikana. Kuna kitu fulani cha kuvutia sana kuhusu yasiyojulikana.
Mara tisa kati ya
kumi, pale unapojifunua kwa mwanaume, baada ya fumbo kuondoka, naye pia
huondoka….atakudondosha kama jiwe la moto! Na haitakuwa kama kuachana kwingine
kokote, itakuwa kama kupewa talaka.
3.
Madhara ya Kimwili
Bado mshahara wa
dhambi ni mauti!
Kuwa mchafu – uko
katika hatari ya magonjwa yasiyo na tiba. Kuna magonjwa saba, nje na ukimwi
ambayo hayana tiba na yote yamebeba madhara ya muda mrefu, na yote huenea na huhusiana
na kundi la watu walio tayari kufanya ngono nje ya usalama wa ndoa!
Utasema yuko tayari
kuwa nami pekee. Usijihakikishie hivyo! Ikiwa wako tayari kufanya ngono nawe,
basi wako tayari pia kufanya na wengine, na huenda wamekwisha kufanya hivyo
tayari.
Unapolala na mtu,
unalala na historia nzima ya ngono ya mtu huyo na KILA MTU ambaye amepata kuwa
naye.
Mshahara wa dhambi
bado ni mauti.
Hatari ya upendo
bandia, madhara ya kimwili na kihisia…
4.
Madhara katika ndoa
Nimewashauri watu
ambao wamekuwa wakisema “ni swa kwetu kufanya ngono kwani tunajua tutaoana”.
Hapana, si sawa…. Kwa nini?
Kwa kuwa Mungu amesema
si sawa…. Nani atakaye kubadili sheria yake? Inawezekana usionane naye!
Kwa wastani, kijana
tineja hupenda takribani mara 10 kabla ya kuingia katika ndoa
Hivyo, hata ikiwa
umeonana naye, umepunguza nafasi za kuwa na ndoa yenye furaha kwa kuwa umemegua
msingi wa uaminifu. Kwenye akili yako, siku zote kutakuwa na lile wazo kuwa mtu
uliyeoana naye anauwezo wa kuwa mdanganyifu. Waliweza kufanya dhambi nawe kabla
ya ndoa, wanaweza kufanya dhambi dhidi yako sasa baada ya kuoana.
Kisha kuna…
5.
Madhara ya kiroho
Lakini Mchungaji,
hauamini kuwa Mungu husamehe? NDIYO, NINAAMINI!
Lakini msamaha na
madhara ni mambo mawili tofauti. Huwa tunadhani mambo yote mawili yanaishi
kwenye mstari mmoja, kuwa tunapousogolea zaidi msamaha ndivyo tunakuwa mbali na
madhara… siyo hivyo!
Daudi alifanya dhambi
na Bathsheba na kisha akafanya amauaji…na katika vifungu viwili vya ajabu vya
Biblia tunaona msamaha wa hali ya juu ambao Daudi aliomba na kupokea – lakini
ngoja niulize, madhara hayakuendelea kuwepo?
Ndiyo. Mungu akasema,
“Daudi, utaishi katika bonde la machozi maisha yako yote. Upanga hautaondoka
nyumbani mwako”
Alimzika mwanae
aliyefariki. Kisha mwanaye mmoja akambaka bintiye. Na Mungu akasema ni matokeo
ya moja kwa moja ya dhambi zake.
Namna gani
ubakie safi?
1.
Linda ufahamu wako
Mlango wa macho na
mlango wa masikio ni muhimu sana…. Ni barabara kuu ya ufahamu.
2 Petro 2:14 “macho
yaliyojaa uzinzi”
Wanaume, lindeni macho
yenu. Biblia inasema (Zaburi 101:3) “Sitaweka mbele ya macho yangu neno la
uovu”. Dai mstari huo
Ayubu alisema
“Nilifanya agano na macho yangu, basi nawezaje kumwangalia msichana kwa
kumtamani?” jiweke mbali na muziki ambao maudhui yake ni tamaa ya kingono.
2.
Usiatamie dhambi
Ikiwa huwezi kuingia
duka la videa na kusalia msafi, usiingie kabisa!
Ikiwa huwezi kuperezi
kwenye vituo vya televisheni pasipo kutazama kitu kichafu, basi zima kabisa.
Ikiwa hamwezi kuwa peke yenu kwenye gari, basi msikae peke yenu.
“Usiupe mwili nafasi”
3.
Azimia kabla
Fanya maamuzi ya awali
kubakia msafi, na kuwa hutaingia kamwe kwenye uhusiano na mtu ambaye hajafanya
maazimio kama hayo.
Maneno ya mpumbavu:
“Atabadilika mara tutakapooana”
Wewe unasema:
“Nimechelewa mno mchungaji” (Tayari nimeshatoa)
Habari njema! Siku
moja mwanamke aliletwa kwa Yesu, akiwa ameshikwa akifanya uzinzi. Alitarajia
kuhukumiwa, lakini Yesu akamwambia, Sikuhukumu, enenda zako na usifanye dhambi
tena!
Huwezi
kubadili yaliyopita, lakini mustakabali wako waweza kuwa bila madoa!
No comments:
Post a Comment