HAPA NI SEHEMU YA KUPATA MAFUNDISHO YALIYOPITA
Na Mchungaji Florian Katunzi
Zipo aina nyingi za maombi yanayotajwa kwenye Biblia takatifu, na yenye matokeo dhahiri yenye kudhihirisha uweza wa ki-Mungu wenye nguvu za kuangusha ngome zote za giza. Katika kitabu hiki nitafundisha aina ya maombi ya kufungua malango na milango.
KUOMBA maana
yake ni Kumwita Mungu. “Katika shida yangu nalimwita BWANA, Na
kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu
kikaingia masikioni mwake.” Zaburi
18:6
Ndani mwa
maombi haya BWANA atakufungulia milango, na hakuna malango
yatakayofungwa mbele yako tena. Neno la Mungu linatuambia:
“Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika
mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya
wafame; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. Nitakwenda
mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande
milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za
gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni
BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.” (Isaya 45:1-3)
Kipindi hiki
wana wa Israeli walikuwa uhamishoni Babeli, kumbuka walitekwa na kuchuliwa
uteka mpaka nchi ya Babeli na Jemadari Nebukadreza, mnamo mwaka 605 KK, baada
ya kuwashinda wamisri katika vita ya Karkameshi. Wakati huo kulikuwa na
makundi mawili yaliyopelekwa uhamishoni Babeli, kundi la pili lilikuwa ni lile
lililochukuliwa mwaka 586 KK.
Huyu
Nebukadneza, ni mtoto wa kiume wa Nabopolasa, aliyemridhi baba yake kuwa
mtawala wa dola ya Wakaldayo mwaka 605 KK. Hii ni kwa mujibu wa kitabu cha The Cambridge Acient history III Uk. 212.
Nebukadireza alikuwa jemadari
kijana aliyekuwa ana misuli ya vita na tena shujaa na mwerevu wa mapigano, hivyo
alikuwa na sifa zote za kurithi kiti cha baba yake.
Wachambuzi wa
mambo ya kale wanamuelezea kuwa alikuwa ni askari na mwanasiasa aliye heshimiwa
sana kutokana na uwezo wake wa kuongoza mapigano na kujenga hoja katika uwanja
wa kisiasa.
Baada ya kutwaa madaraka, mfalme huyu mpya alihusika kujenga vyema himaya na alama za Babeli katika maeneo
mbali mbali ya dunia, tena alijiongezea sifa kwa kumuoa Malkia wa Media Amyhiya, binti wa Cyaxareas, aliyekuwa na
utawala wa Kaskazini.
Neno la Mungu
katika kitabu cha Daniel 2:36-43, linatuonyesha kuwa baada ya Nebukadreza
aliyekuwa kiongozi wa dola yenye nguvu sana ya Ukaldayo kiasi cha ufalme wake unafananishwa na kichwa cha
dhahabu kwa thamani yake, hata hivyo,
alipojiinua kiasi cha kutaka kuabudiwa, ufalme wake, ulikomeshwa na Dola ya
Ukaldayo iliingia hatua ya mwisho pamoja na kuchaguliwa kwa Nabondus mnamo
mwaka 556 KK.
Baada ya kufa
kwa Nebukadreza kinafuata kipindi kifupi cha kupinduana na kuchinjana kwa
watawala na mwisho kabisa utawala wa Dola ya Ukaldayo unafutika kabisa na
unaibuka utawala wa Wamedio, Umedi na Uajemi (Medionapersia) chini ya Mfalme
Koreshi Mwajemi na Dario wa wamedi, walioungana pamoja na kuangusha Dola ya
Ukaldayo mwaka 538. Utawala wa wabanabe ulidumu kwa kipindi cha miakamia mbili
(200), mpaka 331 KK. Ndani ya kipindi
hiki cha utawala wa Wamedi na Wajemi, tunamuona Koreshi, tuliyemsoma katika
andiko letu la msingi akitimiza unabii uliotolewa kwa kinywa cha Nabii Isaya
miaka mia moja hamsini (150) kabla ya kutimizwa kwake katika mwaka 538.
“Katika mwaka wa kwanza wa
Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya
milki ya wakaldayo. Katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Daniel, kwa
kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka ambayo Neno la BWANA lilimjia
Yeremia Nabii, kutimiza ukiwa wa Yerusalem, yaani, miaka sabini. nikamwelekezea
Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwake maombi na dua, pamoja na kufunga na
kuvaa nguo za magunia na majivu.” (Daniel 9:1-3).
Mungu anamuita
Koreshi Masihi (mpakwa mafuta),
kabla ya kuzaliwa kwake, kwani alizaliwa kwa makusudi ya Mungu, japo hakuwa
akimwabudu (Mungu) wala hakuwa mwana wa Israeli, lakini anatumiwa na Mungu
kuyatimiza mapenzi yake, kwa kuwaweka huru
Wayahudi kutoka uhamishoni Babeli.
Koreshi na
mshirika wake Dario walianzisha dola ya Wamedi na Wajemi iliyodumu kwa karne
mbili yaani miaka mia mbili, kama Neno la Mungu linavyosema:
“Ikawa katika
mwaka wa kwanza wa Koreshi Mfalme wa Uajemi, ili kwamba Neno la Bwana alilosema
kwa kinywa cha Nabii Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake
Koreshi, Mfalme wa Waajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote,
akaandika pia akisema Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; BWANA, Mungu wa
mbingu, amenipa falme zote duniani; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika
Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi, kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake,
BWANA, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda,
akajenge nyumba ya Bwana, Mungu wa Israeli, (Yeye ndiye Mungu, aliyoko
Yerusalemu). Na mtu awaye ye yote
aliyesalia mahali popote akaapo hali ya ugeni, na asaidiwe na watu wa mahali
pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali, na
wanyama, zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiayari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya
Mungu iliyoko Yerusalemu.” Ezra 1:1-4
Kudhihirisha
upekee wa Koreshi, anatoa vyombo vya meza ya BWANA ambavyo Nebukadreza
alivitwaa na kuvitia kwenye himaya ya miungu yake. “Tena Koreshi, mfalme, alivitoa
vyombo vya nyumba ya BWANA, alivyokuwa amevileta Nebukadreza toka Yerusalemu na
kuvitia katika nyumba haya miungu yake” Ezra 1:7
Itaendeleaa………
No comments:
Post a Comment