Wednesday, November 23, 2016

MWENENDO WAKATI WA UCHUMBA

Mambo ya kufanya na yasiyofaa kufanya kabla na wakati wa uchumba

Mhandisi Lucas & Happiness Mgalula (TAG City Harvest Church)


Kila mtengenezaji huweka kitabu cha maelekezo ili kuelezea namna ya utumizi wa kitu husika.

Mungu ametupa nguvu na twaenda kwake kujifunza kuhusu udhibiti wa nguvu hizo, Power & Control

Mara nyingi huwa tunaangalia uchumba lakini kuna mahali umeanzia, mahusiano ya urafiki. Tunaangalia namna vijana waliookoka wanavyopaswa kuenenda katika mahusiano kuelekea ndoa.

Umri huu ni kipindi muhimu ambacho hakirudi tena, ni cha muhimu kwako, kwa familia, wazazi, kanisa, jamii nzima na Mungu. Wote wanakutegemea upite salama na kufanikisha kusudi la Mungu.

Kabla ya Uchumba

Kipindi unachojiuliza ikiwa utapata mtu sahihi na ikiwa moyo wako utamkubali. Hata usipoijua njia, hautapotea

I.      Mahusiano na wenzako

-  Fanya ni utaratibu wako kuomba juu ya mahusiano uliyonayo na wenzako ili ule utakaopelekea ndoa ushamiri zaidi na yale yatakayoleta vurugu yafe! Mwanzo 24:12-14 aliyetumwa kumtafutia Yakobo mke alikuwa makini kuomba hivyo
-  Mwambie Mungu akusaidie ili ule uhusiano ulio makini uuone.
-  Anaweza kutokuwa na vigezo vyote unavyovidhania lakini akawa ndiye hasa. Isaya 30:21 Hii ndiyo njia, ifuate

II.  Tafuta ushauri wa wenye hekima wa Mungu

-  Unapoona kama uhusiano mmoja unashamiri na unaweza kupelekea kwenye uchumba, tafuta ushauri wa wenye hekima waliookoka hasa wanandoa.
-  Kuna mambo mengi njiani ambayo utahitaji maombi na msaada wao.
-  Mungu hukupa mwanamke/mwanaume, kazi kwako kumjenga awe mke/mume
-  Hakuna anayekuwa amekamilika, maana hakuna aliyekuwa mume au mke kabla hamjatangazwa hivyo na kuanza kuishi pamoja. Hakuna anayenunuliwa sokoni akiwa kamili
-  Hekima huja kwa kusikia au kupitia, hakuna aliyekuwa amepitia ndoa kabla, hivyo ni vema kupata wanandoa wenye hekima wakusaidie
-  Usiufiche uhusiano wako unaoelekea kwenye uchumba, ni hatari

III.    Kuwachukulia wote kuwa ndugu zako

-  Watu wote unaohusiana nao kanisani na kwingineko, wachukulie kama dada au kaka. Mvulana usiwadharau wadada na msichana usiwachukulie wakaka kama watu waonevu
-  Kuna aina hii ya heshima ambayo kaka na dada wanakuwa nayo kwa kila mmoja. 1Timotheo 5:1-2 Kwa usafi wote, nia, kimawazo, maneno na matendo
-  Sote tu wa damu moja, tumenunuliwa kwa damu ya Kristo
-  Kwa kuhusika katika shughuli nyingi za kanisa zinazoweza kuwaleta pamoja na mkafahamiana, ndipo waweza kujua namna ya kuamua ikiwa tabia zenu zitaendana na mtachukuliana. "Birds of feathers flock together"
-  Baada ya kumfahamu, heshima iendelee, hapa ni kabla ya kuwa “Mr. Special” au “Ms. Special”
-  1Wakorintho 13:4-8 (Sifa za Upendo)
-  Linda moyo wako kuliko vyote ulindavyo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima
-  Kama kuna kitu "special" baina yenu ni bora ukiseme na siyo kuficha ficha. Acheni kung'ang'aniana kama kumbikumbi kila uendako naye yupo halafu mnasema hakuna kinachoendelea baina yenu. Hiyo ni mbaya na hatari na unaweza kukosa "opportunity" na hata kumkosea Mungu.

NOTE: Don't treat anyone special! Don't single her out! Avoid over-clinging to one person when there is nothing-marital material!

Kabla ya Ndoa

-  Usimtembelee mtu wa jinsia tofauti (mchumba) kwake mkiwa peke yenu.
-  Usimfulie, kumpikia au kumsafishia nyumba. Kwa nini upate privileges za ndoa kabla? Una haraka gani?
-  Inaweza kuanza vizuri na kwa nia njema lakini mkaangukia kwenye "premarital sex and pregnancies" ambayo italeta majuto, uchungu na chuki

Wakati wa mahusiano/uchumba

-  Usichochee mapenzi kabla ya wakati wake. Ni mchumba wako lakini haimaanishi unao uhuru wa kufanya lolote utakalo. Huwezi kuwa Rais kabla ya kuapishwa
-  Mwili wako unatambua tayari kwamba huyu ni mtu maalumu, nao unajiandaa na kuitikia hivyo. Kuwa makini.
-  Avoid physical touches, as they will result into premarital sex and unplanned pregnancies
-  Uchumba unaweza kuvunjika. Mungu atakupa amani ndani yako kuendelea mbele, isiwe mzigo kwako ukatumia nguvu nyingi kumridhisha au kumweka kwako halafu mwitikio ukiwa mdogo unaanza kujiuliza kwa nini. Usijilazimishe au kukubali kwa kumhurumia. Ikiwa haiwezekani sema kwa upendo na upole. Ikiwa ana shida, ndiyo maana Mungu akakufunulia wewe ili uchukue hatua za Kikristo kumsaidia

Swali: Vipi kuhusu kutoa zawadi kwa mtu uliye kwenye mahusiano naye/mchumba?
-  Zawadi inaweza kuwa aina fulani ya rushwa, inaufunga moyo wa mtu. Anaweza kukukubali kwa hizo kwa kuwa umeuteka moyo wake na utalazimika kuwa unafanya vitu kwa ajili yake ili aendelee kukukubali

-  Ni bora ukilazimika au kujisikia kutoa zawadi, utoe ambayo haitaumiza moyo wako mambo yakienda kombo. Usianze kununua naye vitu vya thamani, kuwekeza pamoja, kujenga, viwanja na kadhalika.


-  Ni vema upendo ukaja kawaida, zawadi zitafuata kwa nafasi yake

No comments:

Post a Comment