LEO KATIKA MSANII WA WIKI - EMMANUEL LEMBO JR
Rejoice Blog: Labda tuanze kwa kujua majina yako kamili na ikiwa
unatumia jina tofauti kwenye kazi zako za muziki?
Lembo Jr: Jina langu ni Emmanuel Stephen Lembo, ila katika huduma nafahamika
kama Lembo Junior
Lembo Jr |
Rejoice Blog: Je, umeokoka? Unaabudu katika kanisa gani?
Lembo Jr: Nimeokoka nampenda Yesu, kwa sasa naabudu NAIYOTH CHURCH
- GEITA
Rejoice Blog: Historia yako kwa kifupi ya kuimba, yaani ulianzaje na
wapi ulianzia?
Lembo Jr: Naweza sema,nilianzia utotoni sundayschool kids choir...ila
kuingia rasmi kwenye tasnia hii mpaka kuanza kusikika kwa medias ni 2007-2008
nikiwa UDOM
Rejoice Blog: Katika kuimba kwako, je, umeshatoa album yoyote? Majina
ya albamu?
Lembo Jr: Mpaka sasa niko na 4 albums ila tatu ndizo zajulikana
1.TUTEMBELEE. 2 USIFIE JANGWANI. 3.UWE KILA KITU. 4.WINGU LIMESIMAMA WAPI
Rejoice Blog: Wimbo unaoupenda zaidi kati ya nyimbo zako ni upi?
Lembo Jr: mmmmmmh ni almost nyimbo zote nazipenda maana kila wimbo
najua Mungu alinipaje ILA UWE KILA KITU, TUTEMBELEE NA USIFIE JANGWANI ni zaidi
Lembo Jr |
Rejoice Blog: Ni kwa sababu gani unaupenda wimbo huo zaidi?
Lembo Jr: Nyimbo zina ushuhuda mkubwa sana sikuzipewa hivi hivi, nilipitishwa
sana sanaaaaa
Rejoice Blog: Nani anasambaza na kusimamia kazi zako? Na je,
anakusaidia vizuri?
Lembo Jr: Kwa sasa niko na Madam Gisela Malisa, yuko vyema
Rejoice Blog: Ni msanii gani wa muziki wa Injili anayekuvutia na
unapenda kufuatilia kazi zake?
Lembo Jr: Sipho Makhabane, Emmanuel Mgogo
Rejoice Blog: Kuna mafanikio gani umeyapata katika kuimba nyimbo za
Injili?
Lembo Jr: Yako mengi sana kiroho na kimwili. Kiroho; nimekua
nikipokea shuhuda nyingi sana namna nyimbo zangu zimeokoa, zimeponya na kuganga
NAFSI zilizokia zimejeruhiwa. Kimwili kuna kupata kipato ingawa si kikubwa,
ila MUNGU ni mwema. Na pia nimepata EXPOSURE kubwa sana ndani na nje ya mipaka
ya Afrika
Lembo Jr |
Rejoice Blog: Umekutana na changamoto gani katika huduma yako ya
uimbaji?
Lembo Jr: Changamoto ni nyingi sanaaaa kiroho na kimwili pia
kimwili zaidi ni PESA, nitatizo kikubwa, kiroho vita ni KUBWA sana
Rejoice Blog: Unaonaje muziki wa Injili hapa Tanzania? Na hasa wa aina
unayoimba wewe?
Lembo Jr: Muziki huu naona kwa upande wangu uko vyema maana
haujaniangusha
Rejoice Blog: Unatoa ujumbe gani kwa waimbaji wa nyimbo za Injili
ambao kwa njia moja ama nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia
hii?
Lembo Jr: Kikubwa ni kurudi kwenye kusudi la MUNGU na kulitumikia
Shauri la Bwana
Rejoice Blog: Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unakifanya?
Lembo Jr: Kitaaluma nina Bachelor
Degree ya Public Administration (Shahada
ya Sanaa katika Utawala wa Umma), ingawa sijaajiriwa, ninafanya biashara zangu
ndogo ndogo
Rejoice Blog: Je, kimaisha uko wapi? Ndoa na watoto vipi?
Lembo Jr: Naishi na familia yangu Geita, niko na mtoto mmoja tu
Rejoice Blog: Una ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa
Tanzania?
Lembo Jr: Ujumbe TUIFANYE KAZI YA MUNGU KWA UNYENYEKEVU MKUU SANA
Rejoice Blog: Na kwa jamii inayoguswa na kuburudishwa na nyimbo za
Injili una ujumbe gani kwao?
Lembo Jr: Waendelee kutusapoti kwa hali, mali na maombi.
Rejoice Blog: Ahsante sana Lembo Jr kwa muda wako, Mungu akubariki na
kukuinua unavyoendelea kumtumikia kwa uaminifu
Lembo Jr: Nami NIWASHUKURU SANA SANA KWA MUDA WENU NA KUJALI KWENU
MUNGU AWABARIKI SANAAAA
Huyo ndiye Emmanuel Stephen Lembo a.k.a Lembo Junior ambaye umepata kumfahamu zaidi kupitia Msanii wetu wa Wiki. Ukitaka kuendelea kufuatilia habari zake na kazi yake ya huduma, mpate kwa njia zifuatazo:
Emmanuel Lembo Jr:
Instagram:
@lembojr
Facebook:
Lembo Jr Emmanuel
~~~ UMEBARIKIWA! ~~~
No comments:
Post a Comment