RITHA KOMBA KATIKA MSANII WA WIKI
Ritha Komba |
Ni
wiki nyingine tena tunakutana katika “Msanii wa Wiki” na leo tuko na Mwimbaji mwingine
wa nyimbo za Injili anayechipukia, si mwingine bali ni Ritha Komba
Kuna
mengi usiyoyajua kumhusu, lakini leo nafasi ni yako kufahamu angalau machache
zaidi kumhusu yeye. Tujumuike pamoja katika safari hii fupi ya kufahamu Ritha
Komba, msanii wetu wa wiki hii
Rejoice Blog: Je, umeokoka? Wapi unaabudu?
Ritha:
Nimeokoka, naabudu katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Rejoice Blog: Historia yako kwa kifupi ya kuimba, yaani ulianzaje na
wapi ulianzia?
Ritha Komba |
Rejoice Blog: Katika kuimba kwako, je, umeshatoa albamu yoyote? Jina
ya albamu?
Ritha:
Nimeshatoa album audio na video, nasubiri kuizindua tarehe 18 Disemba pale Shalom Eloi Center, Kigamboni Kisiwani ndipo nianze kuisambaza
Rejoice Blog: Albamu yako inaitwaje?
Ritha: Albamu yangu inaitwa 'Mungu
wa Ajabu' na video hii inapatikana YouTube
Rejoice Blog: Wimbo unaoupenda zaidi kati ya nyimbo zako ni upi?
Ritha:
Katika album yangu napenda nyimbo zote, ila unaonibariki sana ni wimbo
wa Usifiwe
Ritha:
Ni wimbo ambao unagusa moyo wangu sana kwa matendo ambayo Mungu
ameyatenda kwangu pasipo mimi kutenda jema lolote
Rejoice Blog: Nani anasambaza na kusimamia kazi zako?
Ritha:
Mpaka sasa bado sijapata msambazaji, nipo kwenye mchakato huo wa kutafuta
msambazaji wa kazi zangu
Rejoice Blog: Ni msanii gani wa muziki wa Injili anayekuvutia zaidi na
unapenda kufuatilia kazi zake?
Ritha:
Navutiwa sana na waimbaji wengi wa Nyimbo za Injili; naweza kusema Angel
Bernard, Jessica Honore BM na Beatrice Mwaipaja. Huwa napenda sana kufuatilia
kazi za hawa waimbaji
Rejoice Blog: Kuna mafanikio yoyote umeyapata katika uimbaji wako?
Ritha:
Mafanikio niliyoyapata ni kuwa msomaji mzuri wa Neno la Mungu na
kujikuta nakuwa mwenye upendo, furaha na amani. Lakini pia najuana na watu
wengi zaidi tofauti na hapo awali
Ritha:
Changamoto ni nyingi hasa kwa sisi ambao tunachipukia, vitu
vingi tunakua hatuvifahamu. Lakini pia suala la uchumi ni
changamoto kubwa sana, kurekodi kunahitaji hela, kutengeneza video nako
kunahitaji hela, matangazo ili kazi iwafikie wengi pia inahitajika
hela. Hizo ni changamoto kubwa nilizoziona
Rejoice Blog: Unaonaje muziki wa Injili hapa Tanzania?
Ritha:
Muziki wa Injili umekua kwa kasi kikubwa sana, sio kama ule wa zama hizo;
mambo yamebadilika. Umekuwa ni muziki wenye ushindani mkubwa. Kwa hiyo
hapo ni kujitoa kwa dhati kuifanya kazi ya Bwana bila kukata tamaa
Rejoice Blog: Unatoa ujumbe gani kwa waimbaji wa nyimbo za Injili
ambao kwa njia moja ama nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia
hii?
Ritha:
Wito ninaotoa mimi ni huu; kama tumejitoa kwa nia ya dhati kuifanya
kazi ya Mungu kupitia uimbaji na iwe hivyo, tusitengeneze makwazo
kwa Muumba wetu
Ritha:
Mimi ni mjasiriamali, nasomea journalism
and media
Rejoice Blog: Je, kimaisha uko wapi? Ndoa na watoto vipi?
Ritha:
Nimeolewa sina mtoto bado
Rejoice Blog: Una ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa
Tanzania?
Ritha:
Ujumbe kwa waimbaji wenzangu, tufanye kazi ya Mungu kwa moyo na tupendane
sisi kwa sisi bila kujali nani anaimba vizuri, nani haimbi vizuri. Tuinuane
maana kwa Mungu hakutaangaliwa sauti yako ilikuaje au umaarufu, bali Mungu
ataangalia tulijitoaje katika kumtumikia yeye
Rejoice Blog: Kwa jamii inayoguswa na kuburudishwa na nyimbo za Injili
una ujumbe gani kwao?
Ritha Komba |
Rejoice Blog: Ahsante sana Ritha kwa muda wako, Mungu akubariki na
kukuinua unavyoendelea kumtumikia kwa uaminifu
Ritha:
Ameen!
Unaweza kuendelea kumfuatilia Ritha Komba katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook, Instagram, YouTube na Twitter
Unaweza pia kuwasiliana naye kwa simu namba 0712496727
Unaweza pia kuwasiliana naye kwa simu namba 0712496727
~~~ Huyo ndiye Ritha Komba, usikose wiki ijayo tena, tunakutana kumfahamu zaidi msanii mwingine. Ubarikiwe! ~~~
No comments:
Post a Comment