Ambele Chapanyota muimbaji wa Nyimbo za Injili anayevuma na wimbo wa Salama Kwa Yesu |
Ambele Chapanyota mwimbaji wa Nyimbo za Injili ambaye anavuma
kwa wimbo wa Salama Kwa Yesu amewataka waimbaji wa Nyimbo za Injili kusimama
katika msimamo wa Neno la Mungu.
Maneno hayo aliyasema Ambele katika mahojiano
aliyoyafanya na Rejoice and Rejoice blog,alipoulizwa anaonaje uimbaji wa Nyimbo
za Injili hapa nchini Tanzania.
Ambele Chapanyota amesikika sana kupitia albamu yake ya
kwanza ya Salama kwa Yesu ambayo ina
nyimbo nane ambazo ni;
Kwasasa Ambele ana Album mbili,zote zimetoka ya pili imebeba jina la Kubali Matokeo yenye nyimbo nane ambayo ni mpya.
Zaidi ya kuimba ni mfanyakazi wa Manispaa Mbeya,anampango wa kufungua bucha na pia ni mwinjilisti.
• Salama
• Yesu
ndie Baraka
• Nakushuru
Mungu
• Unaweza
Yesu
• Nitakuabudu
Bwana
• Nakupenda
Yesu
• Wewe ni
Mungu wangu
• Baba
Mungu
Ziko katika video na audio,
Yeye anabarikiwa sana na wimbo wa Salama kwa Yesu,nikiimba unagusa watu na unanigusa sana mimi
mwenyewe.
Ambele amesema kwamba uimbaji wa Nyimbo za Injili umebadilika
sana hapa karibuni na wengi wameufanya
wa kibiashara zaidi tofauti na jinsi Mungu alivyokusudia.
Katika nchi zingine uimbaji wa Injili uko katika Worship
na Praise, na ndio maana unakuwa unabadilisha watu na hiyo ndio maana halisi ya
kuwepo kwa uimbaji wa Injili.
Amewataka waimbaji wa Injili Kusimama katika msimamo wa
neno la Mungu,tusiyumbishwe na dunia maana sisi ni wahubiri,tufanye kile Mungu
anachotuitia.Tukifanya kitu kizuri jamii itabadilika.
Pia amewataka waimbaji tuwe wabunifu na kufanya
kazi katika ubora.
Zaidi ya kuimba ni mfanyakazi wa Manispaa Mbeya,anampango wa kufungua bucha na pia ni mwinjilisti.
Ambele anaabudu katika kanisa la Mito ya Baraka akiwa
Dar es Salaam na akiwa Mbeya ni EAGT Sabasaba.
No comments:
Post a Comment