Wednesday, June 5, 2013

Rachel Sharp Mtanzania anayemwinua Kristo kwa uimbaji wa nyimbo za Injili nchini Sweden


Rachel Sharp katika pozi
Kama umekuwa ukitembelea blog hii haitakuwa mara ya kwanza kumsikia mwimbaji wa Nyimbo za Injili Rachel Sharp, yeye anaishi Sweden na mwishoni mwa mwaka jana alikuja kuzindua album yake ya Mungu wa Ajabu hapa Tanzania.


Sasa Video ya Mungu wa Ajabu imeshatoka,unaweza kuipata ukamtukuza Bwana Yesu kwa njia ya uimbaji.
Angalia Mungu ni wa Ajabu hapa

Kwa wale wasiomjua Rachel Sharp pamoja na kuimba pia yupo kwenye music team na huongoza sifa na kuabudu katika kanisa la Elim Pentecostal Church Malmö Sweden kanisa linalochungwa na mchungaji Philip Boakye-Agyemang kutoka Ghana.
Ninachompendea Rachel anapenda sana kuvaa Kiafrika,anaitangaza Tanzania na Kiswahili

Pia anaimba na kikundi cha Uinjilisti ambacho kimeunganisha waimbaji kutoka makanisa mbalimbali yaliyopo  Malmö na vitongoji vyake. Ambapo huwa wanahudumu ndani na nje ya nchi ya Sweden.

Mpaka sasa Rachel Sharp anamshukuru Mungu nimeweza kutoa album mbili ambazo ni;
Album ya kwanza ina nyimbo 9. Na imebeba jina la Naringa na Yesu. Nimeimba lugha 3, Kiswahili, kiingereza na kiashanti(Ghana).

Nyimbo zilizomo ni 1. Naringa na Yesu

2, Nikupe nini Bwana

3. Mpe Bwana Utukufu

4. Ooh my father.

5. Thank you Lord

6. Ninakuinua ninakutukuza

7. Bambala

8.father I love

 9. OOh Yesu.

Album hii ilirekodiwa mwaka 2008, kuzinduliwa 2009 Malmö Sweden. Nikisindikizwa na dada Upendo Kilahiro.


 

Album ya pili Imerekodiwa 2011 ina nyimbo 10. Inaitwa Mungu wa Ajabu
Nyimbo zilizomo ni
1. Mungu wa ajabu

2. Only you

3.Ushindi wa Yesu

 4. Yesu anaokoa

5. Wivu

6.Koroiyeye

7. Jesus my Lord

8.Piga baragumu

9.Ascribe

10. Wonderful God.

No comments:

Post a Comment