Monday, January 2, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 2

SIKU YA PILI - 2/2/2017


Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

Walawi 26:9 Nami nitawaelekezea uso  wangu, na kuwapa uzazi mwingi, na kuwaongeza; nami nitalithibitisha  agano langu pamoja nanyi

Mwanzo 17:7 Agano  langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako. 

Kumbukumbu la Torati 8:18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo. 

KUTHIBITISHA AGANO LA MUNGU KWETU KWA UZAZI MWINGI.. KANUNI YA KWANZA YA KUMTAMBUA MTU ALIYE KATIKA AGANO….. NI KUZAA KILA ENEO.. Zaburi 1:3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.

Agano ni la vizazi si mtu mmoja tu. Mwanzo 17:9 Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako.

Mwanzo 9:9 Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu; Mungu akiweka AGANO NA WEWE UJUE NI LA KUDUMU… kizazi chako kitafaidi… 


Kati ya NAMNA YA KUFANYA AGANO NA MUNGU NI KUPITIA DHABIHU.. Zaburi 50:5 Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu

Mungu ili atengeneze agano jipya na wanadamu ~AGANO LA UKOMBOZI WA KUDUMU…. Alimtoa Yesu Kristo kama dhabihu… Je, wewe umetoa dhabihu gani kuweka agano la kudumu na Mungu? Dr. David Oyedepo aliandika Prosperity in the kingdom doesn't answer to fasting, nor does it answer to prayer, or prayer of agreement! It only answers to your understanding and practice of covenant details!

Zaburi 50:5 hapa walikuwa hawakusanywi wacha Mungu wote…bali wale Waliofanya agano na Mungu kwa dhabihu

NB: Omba na kutoa dhabihu… unapoomba maombi ya ki-Agano. SIO KWAMBA MUNGU ANAVUTIWA NA DHABIHU, anavutiwa na utii wa kanuni za agano…. 

ISAKA ALIMPA YEYE HALAFU YEYE TENA AKAMTAKA ISAKA…Mwanzo 22:15-18 Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni akasema, Nimeapa (SIGNATURE) kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES

We are the Standards! 2017

No comments:

Post a Comment