Monday, January 23, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 23

SIKU YA 23 - 23/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

KUSHINDA HABARI MBAYA JUU YA HATIMA YAKO

Mara zote unapokuwa kwenye safari ya maono yako… unaweza kukutana na habari za kuvunja moyo kabisa… WENGI WAMEWAHI KUKWAMA HAPA Ndiyo maana nataka tuombe pamoja… Wakati mwingine habari hizo zinaletwa kwa ubaya na siyo kwamba zina uwezo wa kutukwamisha ila jinsi tunavyopokea ndiyo tatizo… Stamina ya kuchukulia poa habari hizo na kuendelea mbele tena wengine huamua kusita na kuacha kabisa kusonga mbele… 

Angalia watu hawa..

1) JOSHUA NA KALEBU VS. WALE KUMI WENGINE

WATU 12 WALIPEWA KAZI YA UTAFITI/UPELELEZI JUU YA NCHI AMBAYO WANA ISRAELI WALITAKIWA KWENDA… 

RIPOTI YA KWANZA Hesabu 13:26-30 Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi.

Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake.

Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko.

Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani.

Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka.

Hesabu 13:31-33 Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.

RIPOTI YA PILI

Hesabu 13:30 Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka.

Hesabu 14:6-9 Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. Ikiwa Bwana anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, MAANA WAO NI CHAKULA KWETU; UVULI ULIOKUWA JUU YAO UMEONDOLEWA, NAYE BWANA YU PAMOJA NASI; MSIWAOGOPE.

NA WATU WENGI SANA WALIIAMINI ILE HABARI MBAYA ISIYOTIA MOYO…

Hesabu 14:2-4 Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. Mbona Bwana anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri? Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe akida, tukarudi Misri.

Na Mungu naye aliwakasirikia kwa sababa waliamini habari mbaya kuliko ahadi yake…. 

2) NEHEMIA MBELE YA SANBALATI NA TOBIA

NEHEMIA ALIPOANZA PROJECT YA UJENZI WA UKUTA WA YERUSALEMU, HALI HAIKUWA SHWARI… LILIINUKA ZENGWE MOJA MATATA KUTOKA KWA SANBALATI NA TOBIA.. HATUA MOJA BAADA YA NYINGINE… Nehemia 2:19 Lakini waliposikia Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Mtaasi ninyi juu ya mfalme? 

SANBALATI AKAANZA Nehemia 4:1-2 Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi.

Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto?

TOBIA AKAENDELEZA Nehemia 4:3 Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe

PAMOJA NA HAYA YOTE… Nehemia 6:15-16 Basi huo ukuta ukamalizika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, katika muda wa siku hamsini na mbili. Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo makafiri wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tamaa sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na Mungu wetu.

3) PAULO NA WAKATISHA TAMAA

Matendo ya Mitume 21:11-12 Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.

Basi tuliposikia haya, sisi na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda Yerusalemu.

CHANGAMOTO INAYOONEKANA HAPA SIYO UJUMBE KUTOKA KWA NABII LAKINI USHAWISHI WAO WA KUMSIHI AISENDE YERUSALEMU…

PAULO AKASEMA… Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu. Matendo ya Mitume 21:13.. KWA HABARI YA PAULO YESU ALISEMA Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu. Matendo ya Mitume 9:16 

LAKINI PAULO ALISHINDA…NA KWENDA NA PAMOJA NA MATESO ALIYOPITIA ALIFANYA KAZI KUBWA SANA KAMA ALIVYOTAMKIWA NA BWANA KUPITIA ANANIA… Matendo ya Mitume 9:15 Lakini Bwana akamwambia (ANANIA), Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.

MWAKA 2017, MUNGU AKUPE UWEZO WA KUSHINDA KILA ZENGWE LITAKALOINUKA KATIKA JINA LA YESU… USHINDE HABARI MBAYA KAMA YOSHUA NA KALEBU. USHINDE WAKATISHA TAMAA KAMA PAULO, USHINDE WANAODHARAU PROJECT/MAONO YAKO KAMA NEHEMIA… UNABII WA AGABO USIKUZUIE., HABARI ZENYE HITILAFU ZISIKUVUNJE MOYO..ENDELEA KUMWAMINI MUNGU… DHARAU ZA WENYE UCHUNGU ZISIKUONDOE KWENYE MSTARI…. U MSHINDI KATIK JINA LA YESU

UKISHAJUA UNAPOTAKIWA KWENDA, UKISHAJUA NJIA YAKO….UWE MTU USIYEZUILIKA… BE UNSTOPPABLE

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU 

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

No comments:

Post a Comment