Friday, January 20, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 20

SIKU YA 20 - 20/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

KUYAKABILI MAMBO YA SIRI/ATTACKING BEHIND THE SCENE

UNITAKASE NA MAMBO YA SIRI.

Changamoto ya watu wengi ni kuishi vizuri nyuma ya pazia wakati hakuna mtu anayemuona, je umewahi kumuona mtu kabla hajatupa uchafu barabarani anaangalia kwanza ni nani anamuona? KUNA TATIZO mahali…

Hata kama hakuna mtu anayekuona uwe na uhakika Mungu anakuona…. UKIWEZA KUSHINDA UBAYA NYUMA YA PAZIA Ni rahisi kushinda mbele ya kadamnasi…. Ukiingia leo makanisani watu wamebandika BIG G au Bubblish kwenye viti kwa siri bila mtu yeyote kuwaona… HUU NI UGONJWA…. CHARACTER PROBLEM.. Kufanya jambo baya kwa sababu hakuna anayekuona ni hatari sana…

Changamoto ni kwamba MUNGU Huvumbua mambo ya siri tokea gizani, Na hicho kilicho giza tupu huleta mwangani Ayubu 12:22

UKIONA YAMEANDIKWA UJUE YALIVUJA….

2 Wafalme 17:9 Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya Bwana, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma.

LAKINI PIA MUNGU HUZILETA HUKUMUNI SIRI ZA WANADAMU…


Warumi 2:16 katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.

SIYO MATENDO TU HATA MANENO YALIYOSEMWA SIRINI…

Mhubiri 12:14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.

Lakini Luka 12:3 Basi, yo yote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari.

NA NDIO MAANA DAUDI AKAONA ASHUGHULIKIE MAMBO YA SIRI…..

Zaburi 19:12 Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri.

NI VYEMA KUMHESHIMU MUNGU NA KUTENDA WEMA SIRINI NA MWANGANI, USIKU NA MCHANA…KATIKA HALI ZOTE…

MAMBO YAKO YA SIRI YAKIWEKWA WAZI UTAKUWA WA KWANZA KUANGALIA?? KAMA SIVYO… MUOMBE MUNGU AKUTAKASE NA MAMBO YA SIRI SASA NA HATA MILELE….

IKIWA UNATAKA KUFIKA MBALI KWENYE HATIMA YAKO… CHANGAMKIA HILI DILI… Ee BWANA Unitakase na mambo ya siri

ATTACKING YOUR BEHIND THE SCENE WHERE NOBODY SEES…

TUOMBE

Ee BWANA Unitakase na mambo ya siri. Uniepushe na ukaidi ninaujua ambao watu hawajui.. nisikutende dhambi eti kwa sababu hakuna anayeniona. Nisipite njia ya mataifa eti kwa kuwa wenzangu hawapo karibu. Ninaomba niwe mtu wa adili maana Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. (Zaburi 112:4). Mimi ni nuru ya ulimwengu Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza (Yohana 1:5). KILA JAMBO NITAKALOLIFANYA NYUMA YA PAZIA LITAENDANA SAWA SAWA NA MAAGIZO NA UKWELI WA NENO LA MUNGU… Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu. (Zaburi 19:14)

NIMEJIEPUSHA NA MAMBO YA SIRI YASIYOLETA UTUKUFU KATIKA JINA LA YESU………..

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU

MWAKA 2017 NITATEMBEA NURUNI

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

No comments:

Post a Comment