Wednesday, January 25, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 25

SIKU YA 25 - 25/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

BWANA, NISAIDIE KUFANYA MAMBO SAHIHI KWA WAKATI SAHIHI
Umewahi kusikia mtu anaanza biashara ya kuuza sweta wakati wa joto akapata wateja wa kutosha au mtu aliyeuza maua ya Krismasi wakati wa Valentine day? Au Hata kama unataka kusogea na kusonga mbele kwa kasi kiasi gani, hauwezi kupambana kinyume na majira na nyakati ambazo Mungu katika maisha yetu.. Shida siyo nyakati.. ni kutambua wakati uliopo au unaoingia na kusudi la majira au nyakati Mhubiri 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Hii ni kwa sababu huwezi kufanya kitu chochote kikawa kizuri wakati wowote..

Mhubiri 3:11a Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake Sio kwa kutenda tu hata maneno yetu yanafaa SI KILA WAKATI ila kila neno na wakati wake..

Mithali 15:23 Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini! CHANGAMOTO ni pale ambapo hujui majira uliyopo na yakupasayo kufanya ili upate matokeo yatakayoleta SHALOM (Amani, afya, mafanikio, ushindi, n.k) Madahara yake ni kama yale Bwana wetu anayasema juu ya mji huu

Luka 19:44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.

KUTOTAMBUA MAJIRA YA KUJILIWA.. Kwa ufupi, huwezi kufanya maandalizi ya kupokea kitu ambacho hujui kama kinakuja au la…

Luka 19:42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.
Mhubiri akaonyesha madhara ya kuwa na uwezo, hekima, maarifa, uhodari, ufahamu bila kujua namna ya kuunganisha FURSA NA WAKATI….

Mhubiri 9:11 Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.

WAKATI NA BAHATI (FURSA/OPPORTUNITIES) HAZIBAGUI… LAKINI JE, NANI AONAYE JAMBO SAHIHI NA ALIFANYE KWA MUDA SAHIHI?

Danieli 2:21 Yeye (MUNGU) hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa

KWA WAISRAELI ILIBIDI MUNGU AWAWEKEE KABISA KABILA LENYE UWEZO USIO WA KAWAIDA WENYE AKILI za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende

1 Mambo ya Nyakati 12:32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.

EE BWANA, NAOMBA UWEZO WA KUTAMBUA MAJIRA NILIYOPO, WAKATI WANGU, NA FURSA SAHIHI ZA WAKATI HUU, NA KUJUA KIPI CHA KUFANYA NA KIPI CHA KUACHA KWA UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU NA HEKIMA YA MUNGU. NIPE AKILI ZA KUJUA NYAKATI, KUYAJUA YANIPASAYO MIMI NA WATU WANGU TUYATENDE ILI NISICHUKULIWE MATEKA KWA UPOTEVU WOWOTE WA KUTOJUA YANIPASAYO

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

No comments:

Post a Comment