Monday, January 9, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 8

SIKU YA 08 - 08/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA
Zaburi 99:4 Nguvu za mfalme nazo zapenda hukumu; Wewe ndiwe uliyeithibitisha adili; Ulifanya hukumu na haki katika Yakobo.

Zaburi 7:9 Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na viuno Ndiye Mungu aliye mwenye haki.

Amosi 5:15 Yachukieni mabaya; yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni; yamkini kwamba Bwana, Mungu wa majeshi, atawafanyia fadhili mabaki ya Yusufu.

Warumi 10:3 Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.

MUNGU NDIYE ATUPAYE HAKI YETU… NDIYO MAANA TUNASEMA Zaburi 71:2 Kwa haki yako uniponye, uniopoe, Unitegee sikio lako, uniokoe NA IKIWA TULIANGUKA KATIKA MAKOSA NI VYEMA KUOMBA BWANA AKURUDI KWA HAKI YAKE NA SIYO KWA MATENDO YAKO Yeremia 10:24 Ee Bwana, unirudi kwa haki; si kwa hasira yako, usije ukaniangamiza Zaburi 143:11 Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni;

UKITUMIA MATENDO YAKO KUJIHESABIA HAKI NA KUONA KUWA UNASTAHILI… UNAWEZA USIIONE NEEMA YA MUNGU MAISHANI MWAKO HATA SIKU MOJA…

Yakobo 3:18 Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao Amani…

NDIYO MAANA Waebrania 12:14 IMEANDIKWA Tafuteni KWA BIDII kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

MUNGU AKUPE HAKI NA ADILI, UISHI VYEMA KATIKA DUNIA, UPENDEZWE NA UAMINIFU, UFANYE KAZI ZAKO KWA FURAHA BILA KUWA NA UCHUNGU WALA KUJIHUKUMU PAMOJA NA HOFU YA MABAYA YOYOTE… UWE NA AMANI NA WATU WOTE, MUNGU AKUPONYE KWA HAKI YAKE KWANI KWA MATENDO YAKO NA MBINU ZAKO ULISHINDWA KUJIOKOA NA HILA ZA ZA ADUI.. Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni, Ee Bwana, unirudi kwa haki; si kwa hasira yako, usije ukaniangamiza, Kwa haki yako uniponye, uniopoe, Unitegee sikio lako, uniokoe*

Endelea kujiombea………………na kuombea wengine…….HASA WALE AMBAO UNAWAFAHAMU WANAHITAJI NEEMA YA KRISTO
Apostle Shemeji Melayeki

GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES

PHONE: +255 714 548 565

We are the Standards! 2017


No comments:

Post a Comment